Monday, March 5, 2012

KAMPUNI YA BIA TANZANIA (TBL) YADHAMINI MRADI WA MAJI KWA SHULE ZA SEKONDARI 12 MOROGORO



Ofisa Ustawi Jamii Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro, Tabitha Majiku (kulia) akitoa neneo la shukrani baada ya kupokea msaada wa fedha za kusaidia miradi ya maji mkoani humo kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk. Ntobi Mwakibete (wa pili kulia).
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 26.7, Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo kwa ajili ya mradi wa maji kwa shule 12 za sekondari za manispaa hiyo.Kulia ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Uchimbaji Visima vya Maji ya Jae-Hi-Tech Dry Cleaning, Maximillian Makota na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jovis Simbeyi. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 26.7, Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Uchimbaji Visima vya Maji ya Jae-Hi-Tech Dry Cleaning, Maximillian Makota zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya uchimbaji wa visima vya maji mkoani humo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Morogoro.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU