Msanii wa Mziki kutoka South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) kulia akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam jana kuhusu onesho lake la leo litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kushoto ni Msanii aliyeongozana nae Dumiseni Mkihanya.
Msanii wa Mziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo A.K.A Ommy Dimpoz kushoto akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuhusu Onesho lake litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama kulia ni msanii kutoka, South Africa, Cleopas Monyepao (DJ Cloe) na Dumiseni Mkihanya na Meneja wa Kinywaji cha Savana, Diana Musheruzi.
CLEOPAS Monyepao maarufu kama DJ Cleo mkali wa nyimbo ya Facebook kutoka Afrika Kusini kesho anatarajia kutoa burudani katika viwanja vya Posta, Kijitintama Dar es Salaam.
Dj Cleo ameambatana na wachezaji wake Dumisani Makihanya 'Bleksem' na Dj Soul T ambaye amekuwa akionekana katika video mbalimbali za nyimbo zake.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Dj Cleo alisema amefurahishwa sana na ujio wake hapa nchini ikiwa ni kwa mara ya kwanza na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Alisema, anaamini katika onesho lake hilo la kesho atajifunza mengi kutoka kwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kuwajua wanamuziki na muziki wa hapa nchini sambamba na Utamaduni kwa kiasi fulani.
Aliongeza kuwa anahitaji sana kujifunza utamaduni wa Tanzania kwani nchi hizo zinashirikiano mkubwa na zinaendana kwa mambo mbalimbali kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na muonekano wa wananchi wake.
Alisema, kwa upande wa burudani atawapa mashabiki burudani nzuri na ambayo wataridhika nayo ingawa mashabiki wengi wanaujua wimbo wake wa Facebook lakini yeye ananyimbo nyingi hivyo zitakuwa ni 'Supries' kwao.
"Watu wengi wanaujua wimbo wangu wa Facebook lakini zipo nyimbo nyingi ambazo zitakuwa ni mpya kwao na ninaamini watazipenda hivyo waje kwa wingi ili waweze kujionea na kusikia," alisema.
Naye kwa upande wake mmoja wa wanamuziki ambao wataimba jukwaa moja na DJ Cleo, Omari Nyembo 'Ommy Dimpoz' alisema, anajisikia faraja kubwa kupanda jukwaa moja na msanii huyo kwani anaimani naye atajifunza mengi kutoka kwa msanii.
Alisema, kupanda jukwaa moja na wasanii wa nje kunawasaidia muziki wao kufahamika Kimataifa zaidi kwani utajulikana ukilinganisha kazi yake hasa mwanamuziki huyo ni ya Udj.
Sambamba na wanamuziki hao pia jukwaa hilo litapambwa na Suma lee, Dully Sykes, Juma Nature, Tip Top Conection, Wanaume Halisi, Chege na Temba, Wanaume TMK na Wakali Dancers
0 maoni:
Post a Comment