Tuesday, March 20, 2012

MKUTANO MKUU TFF APRILI 21

Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike Machi 24 na 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam umesogezwa mbele hadi Aprili 21 na 22 mwaka huu.
 
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais Leodegar Tenga uliamua kusogeza mbele Mkutano Mkuu kutokana na mtiririko wa matukio ndani ya TFF katika kipindi hicho.
 
Ajenda katika Mkutano Mkuu huo wa kawaida wa TFF kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kuthibitisha muhtasari wa Mkutano Mkuu uliopita, yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita, hotuba ya Rais, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama na kupokea taarifa ya utekelezaji ya Kamati ya Utendaji.
 
Nyingine ni kupitisha taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi wa hesabu na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2012, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya TFF, kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na Wanachama au Kamati ya Utendaji, mengineo na kufunga kikao.
 
MTIBWA SUGAR, SIMBA ZAINGIZA MIL 31/-
Mechi namba 146 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na Simba iliyochezwa Machi 18 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro imeingiza sh. 31,230,000.
 
Jumla ya watazamaji 10,410 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000. Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,763,898.31 kila timu ilipata sh. 6,508,230.51, uwanja sh. 2,169,410.17.
 
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) sh. 867,764.07, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,169,410.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,084,705.08, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 216,941.02 na asilimia 10 ya gharama za mechi sh. 2,169,410.17.
 
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi sh. 120,000 na tiketi sh. 2,480,000.
 
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 728,700 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kilipata sh. 624,600.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU