Mzunguko wa 21 wa Ligi Kuu ya Vodacom unakamilika Machi 21 mwaka huu kwa mechi namba 147 kati ya Villa Squad na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Machi 24 mwaka huu kutakuwa na mechi ya ligi hiyo kati ya Moro United na African Lyon. Mechi hiyo namba 149 itafanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi za Machi 28 mwaka huu ni Ruvu Shooting Stars itakayocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati Moro United itakuwa mwenyeji wa Villa Squad katika mechi namba 153 itakayofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
35 ES SETIF KUWASILI MACHI 21
Kikosi cha watu 35 cha timu ya ES Setif ya Algeria kinatarajiwa kuwasili nchini kesho (Machi 21 mwaka huu) saa 12 alfajiri kwa ndege ya EgyptAir kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba itakayochezwa Machi 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara huo una wachezaji, benchi la ufundi, viongozi wa timu, kiongozi wa msafara kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Algeria (FAF) wakati watatu ni waandishi wa habari.
Wachezaji 20 katika msafara huo ni Mohamed Benhamou, Sofiane Bengorine, Riadh Benchadi, Smain Diss, Farouk Belkaid, Khaled Gourmi, Mourad Delhoum, Said Arroussi, Mokhtar Benmoussa, Tarek Berguiga, Mohamed Aoudi na Amir Karaoui.
Wengine ni Mohamed El Amine Tiouli, Racid Ferrahi, Youcef Ghezzali, Youssef Sofiane, Mokhtar Megueni, Rachid Nadji, Abderrahmane Hachoud na Akram Djahnit. Kocha wa timu hiyo ni Alain Norbert Geiger ambaye ni raia wa Uswisi.
0 maoni:
Post a Comment