Tuesday, March 20, 2012

VURUGU ZILIZOTOKEA KWENYE MCHEZO WA VODACOM PREMIER LEAGUE TAREHE 10/03/2012 KATI YA TIMU YA YANGA NA AZAM


ITAKUMBUKWA YA KWAMBA KWENYE MCHEZO KATI YA TIMU YA YANGA NA AZAM MCHEZO WA VODACOM PREMIER LEAGUE TAREHE 10/03/2012 MWAMUZI WA MCHEZO HUO ISRAEL NKONGO ALIPIGWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA TIMU YA YANGA KATIKA VURUGU ZILIZOTOKEA DAKIKA YA KUMI NA MOJA YAMCHEZO, BAADA YA MWAMUZI HUYO KUFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KUMUONYESHA KADI YA PILI YA MANJANO NA KUFUATIWA NA KADI NYEKUNDU MCHEZAJI WA YANGA HARUNA NIYONZIMA.
 
BAADA YA KUONYESHWA KADI NYEKUNDU MCHEZAJI HUYO BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA HAWAKUKUBALIANA NA ADHABU HIYO NA KUANZISHA VURUGU KWA MWAMUZI ISRAEL NKONGO NA HATA KUDIRIKI KUMPIGA. KATIKA TUKIO HILO LA KUMPIGA MWAMUZI WACHEZAJI WENGINE WALIPEWA KADI NYEKUNDU  NA KUISABABISHIA TIMU YAO KUENDELEA NA MCHEZO WAKIWA NA WACHEZAJI PUNGUFU.
 
KUTOKANA NA TUKIO HILO CHAMA CHAMA CHA WAAMUZI NCHINI FRAT KINALAANI KWA NGUVU ZOTE VITENDO VYA VURUGU VILIVYOFANYWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA KWA VILE VITENDO HIVYO SI VYA KIUANAMICHEZO HASA KATIKA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU, MCHEZO UNAOCHEZWA KWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA MASHINDANO HUSIKA, NA KUWATAKA WACHEZAJI WOTE NCHINI KUTOFANYA KAMA WALIVYOFANYA BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA, KWANI WACHEZAJI HAO WAMEIPAKA MATOPE TIMU YA YANGA KWANI VITENDO HIVYO SI SEHEMU YA HISTORIA BORA YA WACHEZAJI WA TIMU YA YANGA.
 
AIDHA, FRAT INATOA PONGEZI ZA DHATI KWA KAPTENI WA TIMU YA YANGA NA TIMU YA TAIFA SHADRAK MSAJIGWA KWA KUONYESHA UKOMAVU KAMA KAPTENI KWA KUWAZUIA WACHEZAJI WAKE KUTENDA YALE WALIYOKUWA WANAKUSUDIA KUYATENDA PIA KAPTENI HUYO AMENUKULIWA NA VYOMBO VYA HABARI AKIKEMEA VITENDO VILIVYOFANYWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WENZAKE.
 
PIA FRAT INAMPONGEZA KOCHA MKUU WA TIMU YA YANGA KOSTADIN PAPIC KWA KUKEMEA VITENDO VYA WACHEZAJI WAKE NA KUIKEMEA NIDHAMU MBOVU ILIYOONYESHWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA TIMU YAKE.
 
PIA TUNAWAPONGEZA WACHEZAJI WOTE NA DAKTARI WA TIMU YA YANGA,AMBAO KWA NAMNA MOJA WALIJARIBU KWA NGUVU ZOTE KUWAZUIA WACHEZAJI WALIOKUWA NA HALI YA KUMPIGA MWAMUZI WA MCHEZO HUO.
 
VURUGU HIZO ZIMEKEMEWA NA VIONGOZI WA SERIKALI, RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI NA WALE WOTE WANAOPENDA MAENDELEO YA MCHEZO HUO HAPA NCHINI.
 
CHAMA CHETU KINAUNGA MKONO KWA DHATI KAULI ILIYOTOLEWA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI KWA KUKEMEA VITENDO AMBAVYO HAVIKUZI MAENDELEO YA SOKA HAPA NCHINI BALI VINADUMAZA NA KUTUWEKA KATIKA SURA MBAYA KWA WADAU MBALIMBALI WA MCHEZO WA SOKA IKIWA NI PAMOJA NA KUFANYIKA KWA UHARIBIFU WA MALI ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI BILA SABABU ZA MSINGI ZA KUHALALISHA MATENDO HAYO.
 
VITENDO VYA WACHEZAJI HAO VILIWAHI KUTOKEA MIAKA YA AROBAINI NA SABA KATIKA LIGI NDOGO NA SI KWENYE LIGI KUU NCHINI. KWA HIYO WALE WOTE WALIOFANYA VITENDO HIVYO WANAWAJIBIKA KUWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA VITENDO VYAO AMBAVYO VIMETENGENEZA  HISTORIA MBAYA KATIKA LIGI KUU HAPA NCHINI.
 
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU HAPA NCHINI  LIMEWEKA KANUNI NA TARATIBU AMBAZO KAMA TIMU HAIKURIDHIKA NA YALE YANAYOJITOKEZA KWENYE MCHEZO, ZITATAKIWA  KUZIFUATA ILI KUDAI HAKI ZAO NA SI VINGINEVYO.
 
NI IMANI YETU KWAMBA MAFUNZO TULIYOYAPATA KUTOKANA NA TUKIO HILO YATABAKI KUWA SEHEMU YA HISTORIA NA KUTORUDIWA TENA NA TIMU YOYOTE. TIMU YA YANGA NI MIONGONI MWA TIMU KUBWA HAPA NCHINI AMBAPO WACHEZAJI, VIONGOZI NA WAPENZI WAKE WANAPASHWA KUWA MFANO BORA WA KUIGWA NA HILO LINAWEZEKANA ENDAPO KUTAKUWA NA UTASHI WA DHATI WA KUJENGA TIMU BORA NA YENYE KUHESHIMIWA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA.
 
MCHEZAJI MWASIKA MMOJA KATI YA WACHEZAJI WALIOSHIRIKI KUMPIGA MWAMUZI AMENIPIGIA SIMU AKINIOMBA RADHI MIMI  NA WAAMUZI WOTE KWA UJUMLA NA KUNIOMBA NIMSAIDIE KUMUOMBEA MSAMAHA KWA MWAMUZI WA MCHEZO HUO LAKINI HIYO HAITOSHI;NAMSHAURI MCHEZAJI HUYO AJITOKEZE HADHARANI ASIOMBE RADHI KWA SIRI KWANI WALIOATHIRIKA SIKU ILE SI NKONGO PEKE YAKE NI PAMOJA NA WATU WENGINE AMBAO WALIKUJA KUONA MCHEZO WA SOKA NA SI MASUMBWI, NAAMINI MWASIKA ANAJUTIA MAKOSA YAKE NA NI MUUNGWANA, ATAJITOKEZA KUOMBA RADHI HADHARANI  ILI AWE SEHEMU YA JAMII INAYOPENDA MAMBO MEMA.
 
MWISHO NAOMBA VIONGOZI WA YANGA, WAPENZI NA WACHEZAJI,KWAMBA HUU SI WAKATI WA KULUMBANA KWA YALIYOTOKEA BALI NI WAKATI WA KUJISAHIHISHA ILI AIBU ILE ISITOKEE TENA; TUSIPOKEMEA YALE YALIYOJITOKEZA JANA KWENYE UWANJA WA TAIFA KESHO TUTAFANYA VILE VILE KWENYE NCHI ZA WATU, ITAKUWA NI AIBU KWA TAIFA NA SI YANGA PEKEE NA HIYO SI HULUKA YA WATANZANIA.
 
MICHEZO NI FURAHA, UPENDO, UNDUGU, MSHIKAMANO NA KUSHINDANA.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU