Gazetila Tanzania Daima la leo Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika ukurasa wake wa mbele yenyekichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri’, inayodai kumekuwa na mazungumzobaina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusuhatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.
Habarihiyo imedai kuwa Mhe. Pinda anatakamawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini,lakini, imeendelea kudai habari hiyo, “RaisKikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hilini la upepo tu, liachwe litapita”.
Tunachukuanafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania DaimaJumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.
MheshimiwaRais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchiniBrazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzona Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.
Hivisasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma.
MheRais anawasihi wananchi wasiamini habari hizo za upotoshaji zilizomo kwenyegazeti hilo la Tanzania Daima Jumapili.
Piaametoa rai kwa wanahabari wasitoke nje ya mstari wa weledi katika kutekelezakazi zao ili kuendelea kulinda heshima zao binafsi, vyombo wanavyofanyia kazipamoja na taaluma yenyewe.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Aprili, 2012
0 maoni:
Post a Comment