Wednesday, April 4, 2012

UPIGAJIKURA TUZO ZA MUZIKI MWISHO APRILI 6

 Afisa kutoka Kampuni ya uhakiki wa mahesabuya Innovex, Edna Masalu akieleza juu ya utaratibu wa kupiga kura kwenye tunzoza muziki Tanzania wakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaalinalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA. Katikati ni Lloyd Zhungu kutokaInnovex na Mratibu wa Jukwaa hilo, Agnes Kimwaga.
Mratibu wa Tunzo za Muziki Tanzania kutokaBASATA, Bw. Angelo Luhala akisistiza jambo kuhusu tunzo hizo. Pamoja na mambomengine alitoa wito kwa watanzania kuziona tunzo hizo kama kitu chaowanachopaswa kujivunia.
Msanii Khamisi Ramadhan aka H Baba nayealikuwa miongoni mwa wadau wa Jukwaa la Sanaa waliotoa maoni yao kuhusu zoezila upigaji kura kwenye tunzo za muziki Tanzania.
 Mzee Rashid Masimbi ambaye ni moja ya wadauwanaoheshimika kwenye tasnia ya Sanaa nchini akitoa maelekezo na ufafanuzikuhusu tuzo za muziki huku wadau wakimsikiliza kwa umakini.

Zoezi la upigaji kura kwaajili ya kuwapata washindi wa tuzo za muziki Tanzania kwa mwaka 2012 linatarajiakufikia kikomo wiki hii huku wito ukitolewa kwa wadau wa Sanaa kuendelea kuwachaguawasanii wao.

Akizungumza kwenye Jukwaala Sanaa wiki hii makao makuu ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Afisakutoka Kampuni ya ukaguzi na uhakiki wa mahesabu ya Innovex ambayo ndiyo yenyejukumu la kuratibu zoezi zima la upigaji kura Edna Masalu alisema kuwa, mchakatowake unaendelea vema na unatazamia kufika kikomo wiki hii.
 
“Zoezi la upigaji kuralililodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu litafikia mwisho wiki hii Aprili 6,wadau wa muziki wanahamasishwa kuendelea kuwachagua wasanii wenye kazi wanazoonani bora katika kipindi hiki ili kuwawezesha kushinda” alisema Edna.
 
Kuhusu umakini kwenye zoezila kupiga kura, Edna alisema kuwa, Kampuni ya Innovex imebuni njia mbalimbaliza upigaji kura ili kuwawezesha wadau wa Sanaa wa kada mbalimbali kuweza kupatafursa ya kupiga kura na kuwa sehemu ya tuzo hizo zenye umaarufu katika ukandawa Afrika Mashariki na Kati.

Alizitaja njia hizo ambazozinatumika kupiga kura kuwa ni pamoja na ujumbe mfupi wa simu ya mkononikupitia namba maalum, magazeti, vipeperushi na mitandao ya kompyuta ambapoalisisitiza kwamba, kila mtanzania ana haki ya kupiga kura moja tu kwa kilaeneo (category) inayoshindaniwa.
 
“Hakuna njia yoyote yaupendeleo, kura zinapigwa na kuhesabiwa kwa uwazi kupitia mtandao. Toka Academyimeanza hadi sasa zoezi la upigaji kura kwa watanzania mfumo ni wa wazi nahakuna mwanya wa upendeleo” alisisitiza.
 
Awali, akiongea kuhusu tuzohizo, Mratibu kutoka BASATA Angelo Luhala alisema kuwa, wasanii na wadau waSanaa wanapaswa kuthamini tunzo hizo kama kitu chao kwani ni kitu kilichobuniwana watanzania kwa ajili ya kukuza muziki nchini.
 
“Malengo ya tuzo hizi nikukuza muziki nchini na kuwapa ari wasanii wabuni kazi zenye ubora. Ni wazimsanii anayepata fursa ya kuwa kwenye moja ya kipengele kinachoshindaniwa niheshima kubwa” Alisisitiza Luhala.
 
Tuzo za muziki Tanzania kwamwaka 2012 zinatarajia kufikia kilele chake Aprili 14 mwaka huu kwenye Ukumbiwa Mlimani City ambapo wasanii mbalimbali watatambuliwa na kutuzwa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU