Thursday, April 19, 2012

WANACHAMA WA GEPF KULIPA MICHANGO YAO KUPITIA AIRTEL MONEY,

Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia huduma ya Airtel money,halfa fupi ya  uzinduzi huo ulifanyika  katika hotel ya Gold Crest Mwanza. Kushoto ni Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa, akifatiwa na Naibu Waziri wa fedha mh. Gregory Teu,na kaimu mwenyekiti wa bodi bw Ladislaus Salema.
Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia huduma ya Airtel money, uzinduzi huo ulifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika hotel ya Gold Crest Mwanza. Kushoto ni Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa, akifatiwa na Naibu Waziri wa fedha Mh.Gregory Teu,na kaimu mwenyekiti wa bodi bw Ladislaus Salema, kulia ni menaja masoko GEPF Aloyce Ntukamazina, akifatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Daud Msangi akifatiwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng Evarist Ndikiro.
Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa akimshukuru Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal mara baada ya kuzindua mfumo wa malipo ya michango ya wanachama wa GEPF kwa kupitia huduma ya Airtel money, uzinduzi huo ulifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika hotel ya Golden Crest Mwanza. Pichani ni viongozi na wajumbe wa GEPF pamoja washiriki wa halfa hiyo. 
Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa akiongea na waandishi wa habari akifafanua juu ya mpango maalumu uliozinduliwa utakaowawezesha wanachama wa GEPF kulipa michango yao ya mwenzi kwa kupitia huduma ya Airtel money. Halfa ya uzinduzi imefanyika katika hotel ya Gold Crest Mwanza. 
Meneja wa kitengo cha Airtel money Asupya Nalingingwa akielezea huduma za Airtel money na urahisi wa wanachama wa GEPF kuchangia kwa kutumia Airtel money katika halfa ya uzinduzi iliyofanyika katika hotel ya Gold crest, Pichani kulia ni Makamu
wa Rais Dr
Mohamed Gharib Bilal  akisikiliza maelekezo hayo.

MAKUBALIANO HAYO YATAONGEZA UFANISI KWA GEPFNA WANACHAMA WAKE
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Government Employees Pension Fund (GEPF),mfuko wa mafao ya uzeeni kwa watumishi wa serikalini, leo imezindua huduma itayowawezesha wanachama wa mfuko wa GEPF walioko Tanzania nzima kurejesha na kulipa michango yao ya kila mwenzi kwa kupitia huduma ya Airtel money, Uzinduzi wa makubaliano haya yamefanyika leo katika hotel ya Gold Crest mkoani mwanza na kuhudhuria na makamu wa Raisi Dr Mohamed Ghalib Bilalambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi na kushiriki kuzindua huduma hii ya pekee itakayowawezesha wafanyakazi kulipia mafao yao bila usumbufu na kwa ufanisi zaidi.

Katika hotuba yake Mkamu wa Raisi Dr Mohamed Ghalib Bilal alichukua fulsa kuwashukuru Airtel kwa kutoa huduma zinazokithi mahitaji ya jamii na wateja kwa ujumla..aidha dr bilal amewapongeza GEPF kwa kupiga hatua na kutafuta njia mbadala za kuendesha shughuli zake kirahisi kwa ufanisi kwa hakika hatua ya kutafuta changamoyo zilizopo katika ukusanyaji wa malipo, ama kwa hakika hatua mliyoichukue niya kuigwa na vyombo vingine vya umma.

Akizungumza kwa niaba ya Airtel Meneja wa kitengo cha Airtel money Bw Asumpya Naligingwa alisema” Airtel leo tunajisikia furaha sana kugusa maisha ya watanzania kwa njia tofauti kupitia huduma hii ya Airtel money, kama mnavyofahamu kwa kupitia huduma ya Airtel money wateja wetu walioko nchi nzima wanaweza kufanya miamala mbalimbali ya fedha ikiwepo kulipa na kupokea pesa, kulipia Luku, USA visa, kulipia Maji DAWASCO, ada za shule, kununua petrol kwenye vituo kadhaa nchini na nyingine nyingi, leo kwa kushirikiana na wenzetu wa GEPF tunawezesha wafanyakazi na wanachama wote nchi nzima kuweza kurejesha michango yao kwa kupitia huduma ya Airtel money ambayo italeta na kuongeza ufanisi zaidi kwani sasa wateja wa Airtel wanaweza kulipia michango hii wakiwa mahali popote, siku yoyote, wakati wowote na bila usumbufu ”

Tunaamini kabisa ushirikiano huu utaongeza na kuendelea kutunza idadi ya wanachama wa GEPF walioko sasa na kuleta ufanisi katika makusanyo ya michango kwa wanachama. Wenzetu wa GEPF wataweza kuona michango mara tu inapolipwa na pia itarahisisha njia ya malipo na kupunguza idadi ya watu wanaoenda ofisini au bank kulipia hivyo kuokoa muda unaotumika na wanachama kufanya malipo. Jinsi ya kufanya malipo kupitia huduam ya Airtel money ni rahisi mteja anachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye menu ya Airtel money, lipa bill, ingiza jina la fumbo GEPF , ingiza reference namba ambayo ni namba ya uanachama, kisha bonyeza ndio, basi mojakwamoja akaunti ya GEPF itapokea mchango wako na kukutumia ujumbe utakaodhibitisha malipo yako aliongeza Naligingwa.

Naye Meneja masoko wa GEPF bwn Aloyce Ntukamazina alisema” namshukuru makamu wa Raisi Dr Bilal kwa khudhuria halfa hii na kuwa mgeni rasmi wa mkutano wa GEPF mwaka 2012. GEPF kwa kushirikiana na Airtel tumeanzisha mpango utakaotupa sisi GEPF njia ya kukusanya michango ya wanachama ya kila mwezi kwa asilimia kubwa sasa kulinganisha na hapo Awali. Tunawaomba wanachama wetu kutumia njia hii mbadala kufanya malipo yao wakati wowote bila usumbufu wala adha.”

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU