KKamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana leo (Mei 8 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itapanga vituo vya Ligi ya Taifa na tarehe ya kuanza ligi hiyo.
Mikoa nane imeomba kuwa wenyeji wa ligi hiyo itakayochezwa katika vituo vitatu. Mikoa hiyo kupitia kwenye vyama vyao vya mpira wa miguu ni Mikoa iliyoomba vituo ni Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Shinyanga na Singida.
Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni mabingwa wa mikoa. Timu hizo ni Ashanti United ya Ilala (Dar es Salaam), Aston Villa (Singida), Bandari FC (Kagera), CDA (Dodoma), Flamingo SC (Arusha), Forest FC ya Siha (Kilimanjaro), JKT Kanembwa (Kigoma), Korogwe United ya Korogwe (Tanga), Kurugenzi ya Mafinga (Iringa), Lindi SC (Lindi) na Majimaji (Tabora).
Mighty Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers ya Kilombero (Morogoro), Mpanda Stars ya Mpanda (Rukwa), Mwadui FC (Shinyanga), Nangwa VTC (Manyara), Ndanda FC (Mtwara), Pamba SC (Mwanza), Polisi Mara (Mara), Red Coast ya Kinondoni (Dar es Salaam), Super Star ya Bagamoyo (Pwani), Tenende SC (Mbeya) na Tessema FC ya Temeke (Dar es Salaam).
0 maoni:
Post a Comment