SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA (IBF)limemteua Rais wa Shirikisho hilo katikabara la Africa, Onesmo Alfred Ngowi kusimamia pambano la ubingwa wa mabaralinalotambuliwa na IBF.
Mpambano huo utafanyika katika jiji laAccra nchini Ghana tarehe 26 May kati ya bingwa wa mabara wa IBF Emmanuel Tagoewa Ghana na mpinzani wake Antonio De Vitis wa Italy katika uzito wa Junior Lightweight.
Katika mpambano huo wa kutetea mkandawa ubingwa wa IBF ambao unashikiliwa na Emmanuel Tagoe wa Ghana Ngowi atasaidiwana waamuzi wengine kama ifuatavyo: Refarii: Roger Barnor (Ghana). Majaji: Francisco de Ruvo, (Italy), AndrePasquier (France) na Shadrack Acquaye (Ghana).
Mpambano huo uliopewa jina la “NI Sasa au Hakuna Tena” bondia JosephAgbeko wa Ghana atagombea mkanda wa dunia wa Organizesheni ya Ngumi yaKimataifa (IBO) akichuana na bondia Michael Domingo wa Ufilipino katika uzitowa Bantam.
Bondia Josepgh Agbeko anayeishikatika mji wa Bronx katika jiji la NewYork nchiniMarekani atakumbukwa kwenye mpambano wake mkali wa kugombea ubingwa wa IBF katikatika uzito wa Bantam kati yake na bondia Abner Mares wa Mexico tarehe 3 mweziAugusti 2011 katika jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani ambako ilibidiwarudiane mara ya pili baada yakutokea malalamiko ya kuonewa kwa Agbeko.
Hata hivyo bondia Abner Maresalimshinda tena Joseph Agbeko waliporudiana tarehe 18 November 2011 katika jijila California, nchini Marekani.
Naye bondia Joshua Okine wa Ghanaambaye alikuwa bingwa wa mabara wa IBF katika uzito wa Middle kabla ya kupotezaubingwa wake kwa kupandisha uzito atapambana na bondia Theofiilus Teteh pia waGhana kugombea mkanda wa WBO Africa.
Bondia Sammuel Amaoko a.k.a Bruno waGhana atapambana na bondia Sidney Siqueira wa Beazil kugombea mkanda waWBO Africa katika uzito wa Heavyweight.
Mapambano haya yaliyoandaliwa na GoldenMikeBoxing Promotions ya Ghana yatafanyika katika uwanja wa kimataifa wa El-Wak,jijini Accra nchini Ghana chini ya usimamiziwa Mamlaka ya Ngumi zaKulipwaya Ghana (Ghana Boxing Authority, GBA)
Usimamizi wa Ngowi katika mpambanohuu unakuja kipindi kifupi baada ya Francis Cheka wa Tanzania kuunyakua mkandawa IBF Continental Africa Title katikauzito wa Super Middle tarehe 28 Aprilmwaka huu!
0 maoni:
Post a Comment