Sunday, May 13, 2012

TIMU YA TAIFA QUEENS YAIBUKA MSHINDI WA PILI

Mgeni  rasmi,Mama Asha Bilal (pili shoto) na Mama Tundu Pinda kulia wakimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Malawi kwa kuibuka mshindi katika mashindano ya Netiboli ya Afrika yaliyofanyika uwanja wa ndani wa Taifa,jijini dar jana.
Ilikuwa ni shangwe tu mara baada ya mchezo wa netiboli kati ya timu yaTaifa Queens na  Botswana,na hatimaye timu ya Tanzania kuibuka kifua mbele kwa magoli 32 na Botswana kujipatia magoli 23,hivyo kuifanya timu ya Tanzania katika mashindano hayo kunyakuwa nafasi ya mshindi wa pili,huku kinara ikiwa ni timu ya Malawi. 
 Mwenyeji wao mama Tunu Pinda akiongea jambo kwa kuwakaribisha nyumbani kwake wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo, katikati ni mama Asha Bilal na kushoto Anna Bayi mwenyekiti CHANETA.
 Mgeni rasmi,Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika nyumbani kwa Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi kifuta jasho wachezaji wa timu ya Taifa Queens,kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CHANETA,Anna Bayi.
 Mchezaji wa timu ya Netiboli ya Taifa,Taifa Queens,Mwanaid  Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni moja kutoka kwa mgeni rasmi,Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal ikiwa ni sehemu ya kifuta jasho iliyotolewa kwa wachezaji wote wa timu hiyo ikiwa ni ahadi iliyotolewa kutoka kwa Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda,kufuatia timu hiyo kufanya vyema na kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya Netiboli ya Afrika,ambapo katika mashindano hayo timu ya Malawi ilibuka mshindi wa kwanza.
 Mama Tunu Pinda (pili kulia) na wageni mbalimbali wakiburudika kwa namna ya kipekee kabisa.
Timu ya taifa ya Botswana.
Timu ya Taifa Queens.
Mchezaji wa timu ya Botswana akijaribu kufunga goli kwa lango la timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Queens.
Mchezaji wa timu ya Taifa Queens akifunga goli dhidi ya timu ya Botswana,mchezo huo umefanyika ndani ya uwanja wa ndani wa Taifa uliofanyika jana,ampapo Taifa Queens waliibukwa kinara kwa kuifunga timu hiyo goli 32 kwa 23.
Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Queens wakiwa na bendera yao huku wimbo wa Taifa ulipokuwa ukiimbwa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU