LICHA ya kufanyiwa mizengwe ya kila namna na wapinzani wao, Al Ahly Shandy, Simba imesimama imara na kusisitiza itawanyoosha Waarabu hao kesho Jumapili na kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho.
Simba ambayo katika mechi ya awali ilishinda mabao 3-0 jijini Dar es Salaam, inahitaji japo sare kuvuka lakini hata ikifungwa mabao 2-0 itatinga kwenye hatua ya mtoano ambako itavaana na moja ya timu zitakazoenguliwa katika raundi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Miongoni mwa timu maarufu zenye nafasi ya kupangwa na Simba kwenye droo hiyo ni Al Hilal ya Sudan, Maghreb de Fes ya Morocco, AFAD Djekanou ya Ivory Coast, Al Ahly ya Misri, Dynamos ya Zimbabwe, Berekum Chelsea ya Ghana na Al Merreikh ya Sudan.
Kama itashinda kwenye mtoano huo itaingia kwenye makundi ambako kuna fedha nyingi.
Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, alikiri kwamba hali ya hewa ya joto la Shandy ni tatizo, lakini hawana wasiwasi sana kwa kuwa mechi itachezwa saa mbili za usiku.
0 maoni:
Post a Comment