Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo naHabari wa BASATA Godfrey Lebejo akisisitiza jambo wakati akihitimisha programuya Jukwaa la Sanaa wiki hii. Aliwataka wasanii kuongeza thamani katika kaziwanazozalisha.
Mtendaji Mkuu wa asasi ya Musoma HandcraftsHaroun Sabili akitoa elimu kwa Wasanii na Wajasiriamali wa Sanaa za mikonokwenye programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii.
Akina mama Wasanii wa Sanaa za mikonowakiangalia moja ya kazi iliyobuniwa na kuongezewa uthamani. Kazi hiyo ilikuwaimetengenezwa na malighafi kutoka masalia ya viumbe wa baharini.
Msanii akichunguza makini moja ya kazi yaSanaa za mikono.
Mama aking’aa na kazi ya Sanaa za Mikonishingoni kwake.
Sehemu ya Wasanii na Wadau wa Sanaa zaMikono waliohudhuria kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa wiki wakifuatiliadarasa kwa makini.
Huku kukiwa na juhudi zakutambuliwa na kuthaminiwa kazi za wasanii ndani na nje ya nchi, Baraza laSanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kuongeza thamani kwenye kazi zao ilikuzipa ubora zaidi.
Wito huo umetolewa mapemawiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA GodfreyLebejo wakati akihitimisha programu maalum iliyohusu Ubunifu, Utengenezaji naUongezaji thamani katika Kazi za Sanaa kupitia Jukwaa la Sanaa.
Alisema kuwa, ubora katikaSanaa unapatikana pia kwa Wasanii kuangalia wenzao wanafanya nini na wao kupataubunifu mpya kwa kuongeza vionjo, uthamani na ubunifu binafsi katika kuifanyakazi ya Sanaa kwanza kupendwa na baadaye kupewa thamani kubwa sokoni.
“Ni wazi Wasanii wetuwanapaswa kuzingatia uongezaji uthamani kwenye kazi wanazozifanya. Kubuni kazini suala moja lakini kuongeza uthamani katika kazi yako ili ivutie wengi nakuuzika kwa thamani kubwa ni suala lingine la kuzingatia” alisistiza Lebejo.
Aliongeza kuwa, kwa sasakuna taarifa za Wakenya kununua kazi za Wasanii wetu kwa bei ya chini nabaadaye kuziongezea ubunifu, thamani na kuziuza nje kwa bei kubwa. Katika hili anasema, inatokana nawasanii wetu kutokuzingatia falsafa hiyo ya ubunifu na uongezaji thamani wakazi zao.
“Tuna bahati ya kuwa namalighafi nyingi sana, baadhi zimeoneshwa hapa lakini suala hapa ni sisikutumia ipasavyo malighafi hizo katika kubuni kazi zenye ubora na kuhakikishatunazipa thamani stahiki tunapozisafirisha nje” alizidi kusisitiza.
Awali akiendesha darasahilo maalum ambalo wiki hii lilikuwa mahsusi kwa ajili ya wasanii nawajasiriamali wa Sanaa za mikono (Handcrafts), Haroun Sabili kutoka asasi yaMusoma Handcraft alisema kuwa, Sanaa hizo zinahitaji ubunifu na umakini mkubwakwani kinyume chake ni kutokuvutia na kupoteza uthamani.
Alitoa wito kwa Wasaniikujiunga katika vikundi na kuwa rasmi ili kuhakikisha kwanza,wanajengamazingira ya kuwezeshwa lakini pia kupata mafunzo mbalimbali ambayo yatawafanyawazalishe kazi za Sanaa zenye ubora na thamani kubwa.
“Ni ngumu sana kuhudumiamsanii mmoja-mmoja lakini mkiwa kwenye umoja ni rahisi sana kupata fursa zauwezeshaji hususan mafunzo katika kuongeza ubunifu na uthamani wa kazi zenu”alishauri Haroun.
Katika programu hiyoiliyohudhuriwa na wadau 72, elimu kuhusu ubunifu na uongezaji thamani kwenyekazi za Sanaa ilitolewa sambamba na malighafi mbalimbali na jinsi zinavyowezakutumika kuzalisha kazi za mikono kuoneshwa.
0 maoni:
Post a Comment