Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa mahakamani.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka mahakamani hapo.
Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipanda basi la magereza baada ya kesi yake.
Mahakama kuu ya kanda ya Dar es salaam imeamuru mawakili wa pande zote mbili za Mshtakiwa na mlalamikaji kupeleka vielelezo vya umri wa Elizabeth Michael maarufu kama LULU anayetuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya aliekua msanii wa filamu hapa nchini Steven Kanumba ambapo kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Juni 25 mwaka huu.
Mtuhumiwa Elizabeth Michael maarufu ka jina la LULU amefikishwa katika mahakama ya biashara badala ya mahakama kuu kanda ya DSM kutokana na mahakama kuu kuwa katika ukarabati wa majengo yake.
Mara baada ya kuwasili mahakamani hapo majira ya saa tatu na nusu asubuhi Jaji Twaib Fauz anayesikiliza kesi hiyo alieleza kuwa mahakama kuu imekubali kusikiliza kesi ya Elizabeth Michael katika mahakama hiyo baada ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kutupilia mbali ombi lakutaka kesi ya mtuhumiwa isikilizwe mahakama ya watoto kutokana na mtuhumiwa kuwa na umri mdogo.
Jaji Fauz amesema Mahakama Kuu imekubali kusikiliza kesi ya umri wa mtuhumiwa lakini imewataka mawakili wa mtuhumiwa wakiongozwa na wakili Jerome msemwa kupeleka vielelezo vya umri wa mtuhumiwa juni 13 na juni 22 mwaka huu, na kumtaka wakili wa serikali apeleke vielelezo juni 20.
0 maoni:
Post a Comment