Maximo
Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa MARCIO Maximo anatarajia kutua nchini kati ya kesho au kesho kutwa kwa ajili ya kusaini mkataba wa kuinoa klabu ya Yanga.
Msemaji wa Yanga Louis Sendeu amesema ni kweli kocha Maximo amekubali kuja kuifundisha timu ya Yanga na wanaanza naye katika mechi za kombe la KAGAME.
Yanga ambayo ilikuwa ikinolewa na kocha Kostadin Papic waliachana naye katika msimu uliopita wa ligi kuu Tanzania Bara mara baada ya mkataba wake kumalizika.
0 maoni:
Post a Comment