Thursday, June 7, 2012

KIKOSI CHA ENGLAND KIMETUA POLAND TAYARI KWA FAINALI ZA EURO

Msafara wa England ukiongozwa na Meneja wao Roy Hodgson, umetua Nchini Poland tayari kwa FAINALI ZA EURO 2012 zitakazochezwa kwa pamoja Nchini Poland na Ukraine kuanzia Juni 8 na moja kwa moja wakaelekea Krakow kwenye Kambi yao.

Tangu waondoke England na walipotua huko Poland, Msafara wao ulipanda ulipakiwa kwenye Basi

Ingawa Mechi zote za England zitachezwa Nchini Ukraine, England wameamua kuweka Kambi yao Poland na watalazimika kusafiri kwa Ndege jumla ya Maili 5,000 ili kwenda kucheza Mechi zao 3 za Kundi D huko Ukraine.

Katika hatua nyingine kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya England SVEN-GORAN Eriksson anasema wanaomshtumu kocha wa sasa ROY HODGSON kwa kutomchagua Rio Ferdinand kwenye timu wana nia ya kumchafulia jina.

Ferdinand hakuwepo kwenye kikosi cha kwanza kilichotajwa na kocha Roy Hodgson na wakati GARY CAHILL alipopata jeraha, kocha huyo alimuita Martin Kelly mwenye umri wa miaka 22.

HODGSON, ambaye tayari ameiongoza timu hiyo kupata ushindi katika mechi mbili za kirafiki tangu kuchukua uongozi wa timu ya England mwezi uliopita, amesisitiza kuwa kuachwa nje kwa Ferdinand ni kwa sababu za kimchezo wala siyo vinginevyo.

Hata hivyo wengi wanaamini ni kwa nia ya kuepuka matatizo kati yake na JOHN TERRY, ambaye anatarajiwa kufika mahakamani mwezi ujao kwa tuhuma za kumrushia maneno ya ubaguzi wa rangi mdogo wake Ferdinand, Anton, tuhuma ambazo nahodha huyo wa CHELSEA,TERRY anakanusha.


0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU