Thursday, June 7, 2012

TIMU YA TAIFA ZANZIBAR YAENDELEA KUTESA

Timu ya Taifa ya Zanzibar jana iliwatandika Tamil Eelam bao 3-0 katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi B na kufuzu kuingia Nusu Fainali ya KOMBE la DUNIA, rasmi kama VIVA 2012 ambayo ni mahsusi kwa wale ambao si Wanachama wa FIFA ambayo yalishirikisha Timu 9 zilizogawanywa Makundi matatu.

Katika Mechi yao ya kwanza, Zanzibar iliwachapa Raetia [Swiss] bao 6-0.

Nao Darfur, waliokuwa Kundi C, waliendelea na rekodi ya kubandikwa bao nyingi kwani walipigwa 15-0 na Northern Cyprus katika Mechi ya kwanza na kisha kuwashwa bao 18-0 na Provence .

Kwenye Nusu Fainali, Zanzibar watacheza na Northern Cyprus Ijumaa Juni 9 Uwanjani Duhok, Mjini Duhok huko Iraq-Kurdistan.

Nusu Fainali nyingine ni kati ya Wenyeji Iraq-Kurdistan na Provence [France] ambayo pia itachezwa Ijumaa.

Fainali ya Mashindano haya ni Jumamosi Juni 9 Uwanja wa Franso Hariri Mjini Arbil, Iraq-Kurdistan.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU