Meneja wa bia ya Balimi Edith Bebwa kushoto akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa mashindano ya ngoma za asili ya balimi yanayotarajiwa kuanza kwenye mikoa ya kanda ya ziwa june 30 kulia ni meneja masoko wa Tbl Fimbo Buttal.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, jana imezindua rasmi mashindano ya ngoma za asili ya Balimi Extra Lager kwa mwaka 2012. Mashindano haya ambayo yametokea kupendwa sana na wakazi wa kanda ya ziwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika mikoa mbali mbali ya kanda ya ziwa kuanzia Juni 30.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa ikiendesha mashindano haya maarufu kama “Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi Extra Lager” kwa zaidi ya miaka saba sasa , na kwa kweli napenda kusema kuwa ni mashindano yaliyotokea kupendwa sana katika kanda yetu hii ya ziwa,
Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema Bi Edith .
Kwa mwaka huu wa 2012, mashindano yataanza rasmi tarehe 30 Juni katika ngazi za mikoa na kumalizika tarehe 21 Julai. Tutaanza na mkoa wa Mwanza ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora.
0 maoni:
Post a Comment