MchezaRashid Said wa Lindi (kulia) akigombea mpira na mshambuliaji wa timu ya Ilala Innocent Kapuya wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Mchezaji Goodluck Mabiriki wa Ilala (kulia) akigombea mpira na mshambuliaji wa timu ya ya Lindi Khalfan Malibiche wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam
Kikosi cha timu ya wasichana Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza michuano ya Airtel Rising Stars ambapo katika mechi hiyo Mbeya iliifunga timu ya wasicha Arusha 3-2 katika mechi iliyofanyika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam
Kikosi cha Timu ya wasichan Arusha wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza michuano ya Airtel Rising Stars iliyofanyika katika viwanja vya karume jijini Dar es Salaam.
TIMU za soka za mkoa wa Mbeya za wanaume na wanawake zimejihakikishia kucheza nusu fainali ya michuano ya kukuza vipaji wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza leo kwenye uwanja wa Karume, Jijini, Dar es salaam .
Timu hizo zimefuzu kucheza nusu fainali hiyo baada ya kumaliza katika makundi yao zikiwa zinaongoza. Kwa wanawake, Mbeya ilizishinda Arusha kwa bao 3-2 katika mechi ya ufunguzi kabla ya kuichakaza tena Mbeya kwa mabao 4-0, wakati kwa wanaume wao walianza kwa kuishinda Arusha kwa bao 2-1 na kasha kuichapa Kinondoni kwa mabao 1-1.
Timu nyingine ya mkoa wa Arusha nayo imefanikiwa kupitisha timu zake zote za wanaume na wanawake baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi A nyuma ya Mbeya.
Mbali na timu hizo, zingine zilizofuzu kwa upande wa wanaume ni Temeke ilioonyesha kuwa tishio katika michuano hiyo kwa kufunga idadi kubwa ya mabao. Ilianza kwa kuisambaratisha Lindi kwa magoli 12-2 kabla ya kuichakaza tena Ilala kwa mabao 3-0. Wakati wanaume wamefuzu, timu yao ya wanawake inasubiri matokeo kati ya Ilala na Lindi zilizotarajiwa kucheza jana.
Hata hivyo, kwa upande wa wanaume timu ya mwisho itakayoungana na timu hizo inategemea matokeo ya mechi za mwisho za makundi zilizotarajiwa kuchezwa baadaye jana, sambamba na kwa upnade wa wanawake.
Katika mechi zilizochezwa juzi asubuhi timu ya wanawake ya Temeke iliichapa Ilala kwa magoli 2-0. Maholi ya wafungaji yalipatikana katika dakika ya 12 kupitia kwa Madeline Sylvester kunako dakika ya 12 na la pili likiwekwa kimiani na Zuhura Selemani katika dakika ya 44.
Kwa upande wa wanaumke, Temeke iliendeleza mwendo wake wa kugawa dozi baada ya kuibugiza Ilala kwa magoli 3-0. Goli la kwanza la washindi lilifungwa na Khalid Mwenda katika dakika ya 28, la pili liliwekwa kimiani na Paulo Balama katika dakika ya 43 na la mwisho lilpatikana kunako dakika ya 87 kupitia kwa mshambuliaji wake hatari, Bakari Ally.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jioni, timu ya Wanawake ya Arusha iliifunga Kinondoni kwa bao 2-0, Kupitia kwa Anitha Antony katika dakika za 2 na 35. Mechi ya mwisho ilikutanisha Kinondoni na Arusha ambapo zioliztoka sare ya bao 2-2. Wafungaji wa Arusha ni Nazir Abdul katika dakika za 22 na 82, wakati yale ya Kinondoni yaliwekwa kimiani na Omar Ramadhani na Jarufu Lutonga katika dakika ya 55.
0 maoni:
Post a Comment