Friday, June 15, 2012

MCHEZAJI BORA WA MWAKA 2011 SHOMARY KAPOMBE.

Kiungo chipukizi wa Simba SC na Timu ya Taifa (Taifa Stars), Shomary Kapombe (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Sh Milioni 12, kutoka kwa mgeni rasmi katika sherehe za utoaji wa tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Alhaj Ally Hassan Mwinyi (kulia) kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam usiku huu. Kapombe pia alishinda tuzo ya Mwanamichezo Bora chipukizi.Picha na Bin Zubeir Blog
Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka 2011,Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika hafla hiyo usiku huu inayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Wengine pichani Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za TASWA,Masoud Saanane, Mwenyekiti wa TASWA,Juma Pinto na Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Mark Bomani.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akijadili jambo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti,Bw. Richard Wells katika hafla hiyo usiku huu inayoendelea hivi sasa katika ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Simba na Geofrey Nyange (katikati) akiwa katizo hafla hiyo pamoja na Mdau wa simu nyingi wa Michezo nchini,Jamal Rwambo (kulia) pamoja na Maulid Kitenge Makamu Mwenyekiti wa TASWA.
Wadau mbalimbali na waandishi wa habari.
Wageni waalikwa kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia ratiba ya tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Radio Times 100.5 Fm,Rehuru Nyaulawa akimkabidhi tuzo yake mshindi wa tuzo ya mchezo wa Wavu wanawake,Evodia Kazinja.
Mwenyekiti wa TASWA,Juma Pinto akimkabidhi tuzo yake mchezaji bora wa mchezo wa Netiboli Lilian Sylidion kutoka Shule ya Filbert Bayi.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Kim Paulsen akikabidhi tuzo ya mwanamichezo bora wa Olimpiki Maalum,Heri Suleiman.Picha na Full Shangwe Blog.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU