Saturday, June 23, 2012

MWAIPOSA, ISSERE WAMWAGA VIFAA VYA MNICHEZO KIVULE VETERAN.

 Mwenyekiti wa Kivule Veteran wilaya ya Ilala, Jesse John wa TBC Taifa (kushoto) akipokea mipira kutoka kwa mwakilishi wa mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwaiposa katika hafla fupi iliyofganyika jana.
Mkurugenzui wa Issere Sports Abbas Issere akiwa katika picha muda mnchache baada ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti wa timu mpya ya Kivule Veteran, Jesse John hayupo pichani.


MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa ametoa vifaa vya michezo kwa timui mpya ya Kivule Veteran sambamba na mfanyabiasha maarufu wa vifaa vya michezo nchini Abbas Issere kutoa jezi, na mipira.

Akimwakilisha  mbunge wa Ukonga, mume wa mbunge huyo. Ali Mwaiposa alisemna michezo inajenga afya na kuondoa maradhi madogo madogo hiyo aliwashauri kufannya mazoezi.

Naye Issere Sports alisema atahakikisha timu ya Kivule Veteran inapata vifaa vya kutosha na kushiri ki mashindanio mbalimbali ya veteran ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na nje.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU