Thursday, June 28, 2012

TANGA CEMENT WACHANGIA DAMU HOSPITALI YA BOMBO TANGA

 Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Tanga Cement, Amani Shabani akipimwa damu katika zoezi  la uchangiaji damu lililoandaliwa na kampuni hiyo ambapo wafanyakazi zaidi ya 65 walijitolea kuchangia benki ya damu ya Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Katika hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la kiwanda, Pongwe, Tanga jana,  Tanga Cement pia ilikabidhi jokofu la kuhifadhia damu kwa  Kituo Cha Afya cha Rosminian cha Kwalukonge Wilaya ya Korogwe lenye thamani ya shs milioni 9.8. Anayemtoa damu ni  Mteknolojia wa maabara ya Bombo, Yusuf Mgaya.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanga Cement, Injinia Ben Lema (kushoto) akikabidhi jokofu la kuhifadhia damu kwa Meneja wa Kituo Cha Afya cha Rosminian cha Kwalukonge Wilaya ya Korogwe, Padri Ambrose Uhuru Chuwa lenye thamani ya shs milioni 9.8 lililotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu Kitaifa. Hafla hiyo ilifanyika eneo la kiwanda, Pongwe, Tanga jana.
 Ofisa  Mawasiliano wa Tanga Cement, Mtanga Noor akizungumza katika katika zoezi  la uchangiaji damu lililoandaliwa na kampuni hiyo ambapo wafanyakazi zaidi ya 65 walijitolea kuchangia benki ya damu ya Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Katika hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la kiwanda, Pongwe, Tanga jana.
 Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Tanga Cement, Jane Mkony akijiitolea  damu katika zoezi  la uchangiaji damu lililoandaliwa na kampuni hiyo ambapo wafanyakazi zaidi ya 65 walijitolea kuchangia benki ya damu ya Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Katika hafla hiyo iliyofanyika katika eneo la kiwanda, Pongwe, Tanga jana,  Tanga Cement pia ilikabidhi jokofu la kuhifadhia damu kwa  Kituo Cha Afya cha Rosminian cha Kwalukonge Wilaya ya Korogwe lenye thamani ya shs milioni 9.8. Anayemtoa damu ni  Mteknolojia wa maabara ya Bombo, Yusuf Mgaya.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU