Monday, July 30, 2012

AIRTEL YAENDEA KUSAMBAZA MAWASILIANO KANDA YA ZIWA-MWANZA

 Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga akikata utepe kuashira uzinduzi wa mawasiliano uliojengwa na Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, wakwanza kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando. hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
 katikati ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Nyamayinza (kulia) na wakati kushoto ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi mnara wa mawasiliano wa  Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamayinza, Buhunda, Ishoke na Seke, . hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki
 katika alivalia shati la bluu ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa Raisi Mh charles Kitwanga meneja mauzo kanda ya ziwa Galus Mgawe na meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakishangilia na wananchi mara baada ya kukata utepe kuashira uzinduzi wa mawasiliano wa  Airtel nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke, hafla ya uzinduzi wa mnara huu wa ilifanyika katika kijiji cha Nyamayinza
wilayani Misungwi mwishoni mwa wiki.
 Meneja wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw Galus Mgawe akiongea na wananchi mbele ya Naibu Waziri ofisi ya makamu wa Raisi Charles Kitwanga wakati wa uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel wilaya ya Misungwi kijiji cha Nyamayinza, mmnara huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke

Mbele ni Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa raisi Mh Charles Kitwanga na Meneja Mauzo wa Airtel wakiwa wamejiunga wananchi wakiserebuka ngoma ya asili kufurahia uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel wilayani Misungwi. mmnara huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na Seke


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi ashauri Wananchi wa nyamayinza, “tumieni fulsa ya mawasiliano haya ya Airtel kwa kuendesha shughuli za masoko”


Mtandao huo wa Airtel kurahisisha upatikanaji wa huduma zake zote kama intaneti, Airtel Money na kupiga simu vijiji vya  Nyamainza, Buhunda, Ishoke na SekeMwishoni mwa wiki hii Mwanza Airtel Tanzania imezindua mtambo kabambe wa mawasilano katika mkoa wa kanda ya Ziwa nje kidogo ya mkoa wa Mwanza katika wilaya ya Misungwi ikiwa ni mkakati wa Airtel uliojiwekea katika kuendelea kufikisha huduma zao bora  vijijini Akizindua mnara huo mpya Naibu mwishoni mwa wiki Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Raisi Mhe, Charles Kitwanga (mawe matatu) amesema Maendeleo vijijini yatakuwakwa kasi sana iwapo wananchi watatumia mawasiliano ya simu za mkononi kutafuta masoko ya madini, mifugo au vyakula wanavyozalisha  sehemu mbalimbali Waziri kitwanga alibainisha hayo katika kijiji cha Nyamayinza kata ya Gulumungu wilaya ya Misugwi Mkoani Mwanza wakati akiongea na wananchi na kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya Airtel Tanzania.Alisema “Mawasiliano yanafaida kubwa sana duniani na ndio hufanya maendeleo ya jamii kwenda kwa kasi, hivyo wananchi wa vijiji vyote vinavyoizunguka nyamayinza tumieni fulsa ya kupata mawasiliano haya ya Airtel kwa kuendesha au kuendeleza biashara zenu,pia anzisheni biashara za kutuma na kupokea pesa za Airtel Money  na mtumie mawasiliano haya haya pia kutafuta wateja wakutosha katika bidhaa za kilimo na mifugo mnazozalisha”
Nae Meneja mauzo wa Airtel Kanda ya Ziwa Bw, Galus Mgawe akiongea kwaniaba ya mkurugenzi wa Airtel Tanzania, alisema “Airtel kwa kukamilisha dhamira yetu ya kutoa mawasiliano yenye uhakika kwa mwaka huu tunaanza na kuzindua wa mtambo huu wa mawasiliano hapa wilayani Misungwi utakaowezesha zaidi ya watu 15,000 waliopo vijiji vya Nyamainza, Buhunda, Ishokela, na Seke kuwasiliana na ndugu na jamaa kwa uhakika wakiwa Airtel Kupatikana kwa mtandao huu wa Airtel pia kutasaidia wakazi wa vijiji vyote na jirani  kufurahia huduma zote za Airtel ikiwemo ile ya Airtel Money, kutuma na kupokea sms, pamoja na kufurahia mtandao bora na nafuu wa Intaneti.Uboreshwaji na uwekaji wa Minara ya mawasiliano ya Airtel katika vijiji unawezeshwa kwa ushirikiano na serikali na mamlaka za mawasiliano nchini kwa kuwa imetuwekea mikakati bora zaidi wakati wa uwekaji wa miundo mbinu hii ya mawasiliano kila mahali Akiongezea kuhusiana na mpango wa kusambaza mtandao unaoendelea alisema Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw Jackson Mmbando alisema “kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za mawasiliano kutokana na mazingira au kupanuka kwa shughuli za jamii husika ndio yanayotufanya Airtel kuitikia wito na kutanua zaidi wigo wa mtandao wetu kwa eneo husika.“Huduma ya mawasiliano imekuwa moja kati ya nyenzo muhimu katika kuwezesha shughuli nyingi za kijamii  nchini Tanzania na duniani kote, kupanuka na kufikisha mawasiliano vijijini ni chachu ya kukua kwa uchumi na kuwezesha jamii iliyopo maeneo hayo kupata miundo mbinu mbadala katika shughuli za uzalishaji Airtel bado tunategemea kuendelea kupata ushirikiano wa kutosha kati yetu na serikali  katika kuhakikisha tunafikisha mawasiliano vijijini
kwa kutuwekea mfumo bora wa kulipa kodi na kupata vibali vya kuweka mitambo ya mawasiliano ili kufaidisha jamii.Airtel ni mtandao bora ulioenea zaidi na kutoa mawasiliano nchini kote kwa kufikisha  mawasiliano ya uhakikia kwa takribani asilinia 85 kwenye maeneo ya miji na vijiji nchini Tanzania.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU