Wednesday, July 18, 2012

AIRTEL YAJA NA KOPA NA UDAKE SALIO

 Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya “Daka Salio” iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel , pichani kushoto ni Afisa uhusiano wa Airtel na kulia ni Meneja bidhaa wa Airtel Salim Madati
 Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akifafanua kuhusu huduma ya mpya ya “Daka Salio” wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Moroco na kuhudhuria  na waandishi wa habari, katika ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akifatiwa na Meneja Bidhaa Salim Madati
Maafisa wa Airtel kwa pamoja wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya “Daka Salio” wakati wa uzinduzi Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Moroco na kuhudhuria  na waandishi wa habari, kutoka kushoto ni Afisa mawasiliano na matukio Bi Dangio Kaniki, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando na Meneja Bidhaa Salim Madati


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuendeleza dhamira yao ya Uhuru wa kuongea imetoa fulsa nyingine kwa wateja wake kwa kuzindua huduma kabambe ya Daka salio ikiwa ni jitihada zake katika kutimiza dhamira yake ya kuendelea kutoa uhuru wa kuongea kwa wateja wake nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando by Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kuleta huduma hii ya Daka salio kwa wateja wetu wote waendelee kufurahia huduma zetu kila wakati, ikiwa sasa unaweza kukopa na kuongea na ndugu au rafiki wa mtandao wowote sasa hakunakubeep tena.

Hii ni huduma nzuri kwa familia, marafiki ndugu au jamaa kwa kuwa itaondoa tatizo la watu kubeep, Airtel tunasema kwanini ubeep au uteseke kukopa kiwango kikubwa na kulipa zaidi.  Daka salio kidogo na ulipie kidogo na airtel. Ili kufurahia huduma hii ni rahisi na haraka tuma tu neno daka kwenda 15549.  Uongee mwanzo mwisho, kwa raha zako.

Mteja yeyote anaweza kukopa ikiwa tu amekuwa mteja wa Airtel kwa mfululizosiku tisini, awe anasalio la hadi shilingi 50 na asiwe anadaiwa deni la Daka salio ikiwa alishakopa kupitia huduma hii.

Faida ya kukopa salio ya Airtel ni kwamba tunakukopesha kiwango kidogo ambacho utalipia kiduchu tu na utaongea kwa muda mrefu. Achana na wanaokopesha kiwango kikubwa halafu unaongea kidogo.

Mteja wa Airtel anaekopa salio kwa daka salio ataweza kukopa sh 180 na akitaka kulipa atalipa ziada ya sh 18 tu yaani atatoa jumla ya 198 tu, kwa hiyo hata ukiongeza salio la sh 500 bado utabakia na salio la kukuwezesha kufurahia uhuru wa kuongea toka Airtel.

Airtel  imekuwa na ubunifu wa bidhaa na huduma zake zaidi  kwa lengo la kufaidisha jamii kwa ujumla. Hivi karibuni ilizindua huduma ya SUPA 5 yenye dili tano bomba na inaendelea kutoa unafuu kwa wateja wa Airtel kupata sms 200 bure, kuongea na watu watatu kwa nusu shilingi siku nzima,  kupata huduma ya facebook bure , intaneti bure usiku, pamoja na kongea kwa robo shilingi nyakati za usiku kwa kupiga tu*149*99# na kufuata utaratibu.

Airtel pia kupitia huduma yake ya Airtel money inawawezesha wajasiliamali waliowekeza katika kwa kuwa wakala wake nchi nzima pamoja na wateja wake,  kwa wateja sasa wanapata  mara mbili ya salio wanaloongeza kupitia huduma ya Airtel Moneywakati  WAKALA wote nchi nzima watapata mara mbili ya kamisheni zao kwa mwezi juni - julai kwa mihamala yote watakayofanya kupitia Airtel Money.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU