Thursday, July 26, 2012

HATIMAE YANGA YATINGA FAINALI ZA KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUITANDIKA APR 1-0

 Kiiza akipambana na mchezaji wa APR
 Wachezaji wa yanga wakishangilia walipopata bao
 Said Bahanuzi 'Spider Man' akiwa amembeba Kiiza baada ya kufunga bao
Kiiza akipambana

BAO pekee la mwanasoka bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 110, limeipa Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo, na sasa itamenyana na Azam FC keshokutwa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Kiiza alifunga bao hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna Niyonzima ambaye alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia maamuzi ya refa, baada ya Kiiza kuangushwa.
 
Yanga waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo. Dakika tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.

1 maoni:

Anonymous said...

hongereni sana wachezaji wote wa yanga.huu ni mwanzo wa mafanikio kwani kesho tunaenda kumaliza kazi.viongozi yanga wawe makini na mbinu za nje ya uwanja pamoja na refa.Pia John Boko anahitaji ulinzi mkali kwani amekuwa akitufunga mabao kwa urahisi sana,na pia ndiye tegemeo la Azam kwa ufungaji na akibanwa yeye hakuna mtu mwingine wa kutusumbua

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU