Mpira nyavuni
Wakati wachezaji wa Azam wakishangilia bao lililofungwa na John Bocco
NUSU Fainali ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano inayodhaminiwa na Super Sport na Azam, imemalizika kwa Azam FC kuitoa AS Vita kwa kuifunga mabao 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, AS Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Mfongang Alfred dakika ya 34, baada ya kuunasa mpira uliopigwa na Ibrahim Shikanda na kuichambua ngome ya Azam kabla ya kufumua shuti kali lililomshinda kipa Deo Munishi ‘Dida’.
Vita walipata pigo dakika ya 41, baada ya mchezaji wao, Issama Mpeko kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Azam ilisawazisha bao hilo, kupitia kwa John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 68 aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Kipre Tchetche kutoka wingi ya kulia.
Mrisho Khalfan Ngassa aliyeingia kutokea benchi kipindi cha pili aliifungia Azam bao la ushindi dakika ya 89, akimalizia pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’. Baada ya kufunga bao hilo, Mrisho alikwenda moja kwa moja kwan mashabiki wa Yanga na kushangilia nao, badala ya mashabiki wa Azam.
Nusu Fainali ya pili kati ya mabingwa watetezi, Yanga na APR ya Rwanda ndio inaendelea hivi sasa na mshindi atamenyana na Azam. Azam inakuwa timu ya pili nje ya Simba na Yanga kuingia Fainali ya michuano hii, baada ya mwaka 2006 Moro United kufanya hivyo.
0 maoni:
Post a Comment