Awali Shirikisho la Filamu Tanzania – TAFF, linawashukuru waandishi wote wa habari za michezo na burudani pamoja na vyombo vya habari kwa ujumla kwa jitihada zenu za ukuzaji wa shughuli za sanaa hapa nchini pamoja kuchagiza changamoto mbali mbali na kuibua fursa zilizo jificha na zile zilizo wazi kwa lengo la kuleta maendeleo na hasa kwa tasnia ya filamu Tanzania tunawa pongeza sana kwa jitihada mnazozifanya.
Ndugu Waandishi kama mnavyofahamu kwamba taasisi isiyo na mipango haiwezi kupiga hatua nyingine kutoka mahali ilipo lakini pia taasisi isiyo kuwa na mkakati haitajua inaelekea wapi?
Kutokana na sababu hizo na nyinginezo TAFF imeandaa Semina ya siku mbili kwa ajili ya kutayarisha mpango Mkakati wa miaka mitano ijayo. Semina hiyo itafanyika katika ukumbi wa Ofisi za TCRA Jengo la Mawasiliano Towers ubungo kuanzia saa 3 asubuhi tarehe 30 – 31, Julai 2012.
Ndugu Waandishi semina hiyo inafuatia baada ya kufanyika ya awamu ya kwanza ambayo ilifanyika 28 – 20 May 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya White Mark iliyopo eneo la Ubungo Plazza Mjini Dar es Salaam.
Aidha Wajumbe wataohudhuria semina hiyo wanatoka taasisi za Benki za N.M.B, CRDB , Backelys Bank, Bank of India, TRA , TCRA, TBS, NSSF , Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Bodi ya Filamu Tanzania, BASATA, COSOTA, ITV Equity Bank, European Union, Foundation for Civil Society, Ubalozi wa Sweden, Uholanzi, US – AID, Global Publishers, UNESCO, UNICEF, TGNP, T.I.B Mpigile Company , Wizara ya Viwanda Biashara, Tigo, Vodacom, TBL, ADB, TWAWEZA, Ubalozi wa Canada, Ubalozi wa Ufaransa , Ubalozi wa Denmark ,Wasanii kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Mwanza,Pwani na Dodoma..
Malengo ya Semina hiyo ni kujadili na kuweka utekelezaji wa vipaumbele muhimu vya utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la Filamu.
Ndugu Waandishi lakini pia natumia fursa hii kuwakaribisha kwa ajili uchukuaji wa habari kadri mtavyoweza wakati wa semina hiyo.
Ahsante
Nawashukuru nategemea ushirikiano wenu.
WILSON R. MAKUBI
KATIBU MTENDAJI.
0 maoni:
Post a Comment