Thursday, July 12, 2012

KOCHA YANGA ATANGAZA KIKOSI CHA WACHEZAJI ISHIRINI KWAAJILI YA KOMBE LA KAGAME AMTEMA SHADRACK NSAJIGWA


KOCHA wa YANGA TOM SAINTIEF ametangaza kikosi cha wachezaji ISHIRINI watakaoshiriki katika mashindano ya vilabu kwa nchi za afrika mashariki na kati ya KAGAME, huku nyota wake chipukizi SAIMON MSUVU, FRANK DOMAYO na OMEGA SEME wakiwa hawapo katika kikosi hicho kutokana na kuwa na majukumu kwenye kikosi cha timu ya taifa NGORONGORO HEROES inayojiandaa kuivaa NIGERIA.

Mabadiliko mengine aliyoyafanya kocha TOM ni kutomtumia nahodha wa YANGA, SHADRACK MSAJIGWA katika mashindano hayo ambapo ameamua kumpumzisha ili ajiandae na ligi kuu ya TANZANIA BARA inayoanza mwezi SEMPTEMBA mwaka huu..

Akizungumzia mchezo wa ufunguzi kocha TOM amesema timu yake imejiandaa vizuri na mchezo  ufunguzi  ya dhidi ya ATLETICO ya BURUNDI utakaokuwa mchezo wa pili wa ufunguzi utakaochezwa jumamosi 2030.

Kocha aliwataja wa baadhi ya wachezaji kuwa ni MAKIPA YOW BERKO, ALLY MUSTAPHER, KERVIN YONDANI, NADIR HARUB KANAVARO, JUMA ABUU GODFREY TAITA,  STEPHANO MWASIKA, ATHUMAN IDD,RASHID GUMBO,JUMA SELF, NIZAR KHALUFAN,  IDRISA RASHID, HAMIS KIIZA, SAID, JERRY TEGETE, SHAMTE ALLY na HARUNA

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU