Friday, July 13, 2012

MWANZA YATINGA FAINALI COPA COCA-COLA 2012

Mwanza imejipatia tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Julai 13 mwaka huu) kuilaza Temeke mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Hadi dakika 90 za kawaida zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1. Mwanza walitangulia kufunga dakika ya tatu kupitia kwa Jamal Mtegeta kabla ya Temeke kusawazisha kwa penalti dakika ya 56 iliyowekwa wavuni na Baraka Ntalukundo.

Mabao mengine ya Mwanza yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali keshokutwa (Jumapili) yalifunga katika dakika 30 za nyongeza. Mtegeta alitikisa wazu dakika ya 94 kabla ya Dickson Ambundo kukwamisha la tatu dakika ya 108.

Nusu fainali ya pili itachezwa leo jioni ikikutanisha timu za Morogoro ambayo kwenye robo fainali iliibamiza Mara mabao 4-0 na Tanga iliyopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU