Thursday, July 19, 2012

NBC YAMKARIBISHA BOSI WA BARCLAYS AFRIKA NA KUFANYA MAZUNGUZO NA WATEJA WAO.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza wakishakana mikono wakati wa hafla iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wa makampuni jijini Dar es Salaam jana
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili kushoto) katika  hafla iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wa makampuni jijini Dar es Salaam jana.  Wa pili kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Kennedy Bungani na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa makampuni wa NBC, Minnie Adolf Kibuta. Bwana Bungani awali alifanya mazungumzo na wafanyakazi wa NBC nchini ili kufahamiana nao.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Kennedy Bungani (kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza katika  hafla iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake wa makampuni jijini Dar es Salaam jana.  Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru. Bwana Bungani awali alifanya mazungumzo na wafanyakazi wa NBC nchini ili kufahamiana nao.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Kennedy Bungani (wa tatu kushoto) akipiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC Tanzania baada ya kufanya nao mazungumzo na baadhi ya wateja wa makampuni wa NBC jijini Dar es Salaam jana usiku.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Kennedy Bungani (kushoto) akipiga picha na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula Mfugale (katikati) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Godfrey Ndalahwa  baada ya kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa benki hiyo na baadhi ya wateja wa makampuni wa NBC jijini Dar es Salaam jana usiku.

 Mshauri wa Mahusiano wa NBC, Eddie Mhina (kulia), Meneja Chapa na Matangazo, Aden Kitomari (kushoto), pamoja na mfanyakazi mwingine wa benki hiyo wakiwa katika hafla waliyoandaa kwa wateja wao wa makampuni
jijini Dar es Salaam jana.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU