Mkamu mwenyekiti wa SIMBA KABURU akionyesha mkataba wa OKWI ambaye bado ana mkataba wa kuichezea timu hiyo .Simba umesikitishwa na habari zilizovumishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda kujiunga na wapinzani wa jadi, Yanga SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, alisema kwamba habari hizo hazina ukweli wowote, ni kinyume cha maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na zina lengo la kupotosha ukweli na kuwanyima raha wale wote wenye mapenzi mema na Simba.
0 maoni:
Post a Comment