Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeteua waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.
Waamuzi hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu kwa ajili ya vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12 na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa CECAFA.
Kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).
0 maoni:
Post a Comment