Tuesday, July 24, 2012

TAASISI YA JANE GOODAL YAZINDUA MRADI WA MITI

 Muasisi wa Taasisi ya Jane Goodall, Dk Jane Goodall (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa  kampuni ya Saruji ya Twiga Cement (TPCC), Pascal Lesoinne wakitembelea kitalu cha miti wakati wa halfa ya uzinduzi wa mradi wa miti wa kukarabati na kuasilisha machimbo ya saruji ya kampuni hiyo uliofanyika Wazo Hill, nje kidogo ya Jiji la
Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Twiga Cement  (TPCC) wakimwangalia mwanaserere sokwe wa Dk Jane Goodall wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa miti wa kukarabati na kuasilisha machimbo ya saruji ya kampuni hiyo, uliofanyika Wazo Hill, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Boko na ambaye pia ni mwanachama wa Roots and Shoots akipanda mti wakati wa halfa ya uzinduzi wa mradi wa miti wa kukarabati na kuasilisha machimbo ya saruji ya kampuni  ya
Twiga Cement (TPCC) uliofanyika Wazo Hill, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga Cement, Ekwabi Majigo (kulia) na Mkuu wa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Jayne Nyimbo wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za Boko na Maendeleo,  wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa miti wa kukarabati na kuasilisha machimbo ya saruji ya kampuni hiyo, uliofanyika Wazo Hill, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo.
Muasisi wa Taasisi ya Jane Goodall, Dk Jane Goodall (wa nne kushoto, waliosimama), Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kushoto kwake) na Meneja Mazingira wa kampuni hiyo, Juliet Mboneko (wa sita kushoto) wakipozi kwa picha na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Twiga Cement katika halfa ya uzinduzi wa mradi huo.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU