Friday, July 20, 2012

YANGA YAFANYA MAUAJI YAITANDIKA APR BAO 2-0

Nizar Khalfan wa Yanga akiwachambua mabeki wa APR.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kuongoza lililofungwa na Said Bahanuz dakika ya 28 ya mchezo kipindi cha kwanza,huku mwamuzi wa mchezo huo akiwataka kurudi uwanjani.


Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga, leo wamepata ushindi wa kishindo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam walipoitwanga Timu ngumu APR bao 2-0 huku bao zote zikifungwa na Said Bahanuzi katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi C la Mashindano ya kugombea Kagame Cup, Klabu Bingwa ya Afrika ya Mashariki na Kati, dhidi ya APR ya Rwanda.

Bao za Bahanuzi zilifungwa katika Dakika ya 22 na 66 na kuifanya Yanga imalize Kundi C ikiwa nafasi ya Pili na Robo Fainali itacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi B ambae atakuwa mmoja kati ya Azam, Tusker au Mafunzo.

Kabla ya Mechi ya Yanga leo kulitangulia Mechi ya Kundi A kati ya Ports ya Djibouti na URA ya Uganda ambayo URA ilishinda bao 3-1 na hivyo kuitupa nje Ports ambayo imemaliza Mashindano ikiwa imefungwa Mechi zake zote tatu.

Matokeo hayo yamezifanya Timu za URA, Vita na Simba ndizo ziingie Robo Fainali.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU