Thursday, August 2, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA KISAWASA SECONDARY SCHOOL ILIYOPO MOROGORO

 Kisawasawa Secondary School Headmaster in Morogoro, Menasi Msigwa
receiving books donation from Dangio Kaniki Airtel Public relations
and Event Officer second while from left looking on is Airtel Public
relations and Event Officer Dangio Kaniki.
Airtel Public relations and Event officer Dangio Kaniki left
challenging one of the students in Kisawasawa Secondary School during
the book handover ceremony held at Kisawasawa Secondary school in
Morogoro, behind left is Corporate Social and Responsibility Manager
Hawa Bayuni, second left is Headmaster of Kisawasawa Secondary School
Menasi Msigwa followed by Airtel Sales Officer Mohammed Mbamba.
Airtel Public Relations and Event Officer Dangio Kaniki (left) making
a point during the book handover ceremony in Kisawasawa Secondary
School in Morogoro, left is the Corporate Social and Responsibility
Manager Hawa Bayuni and right is the Headmaster of Kisawasawa Primary
School Menasi Msigwa.

 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kupitia mpango wake wa 'Airtel shule yetu' imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule ya sekondari Kisawasawa ya mkoani Morogoro lengo likiwa ni kusaidia
maendeleo ya elimu mkoani hapo na kutoa huduma kwa jamii.

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika shule ya sekondari
Kisawasawa  na kuhudhuriwa na  wawakilishi wa shule, wanafunzi,
waandishi wa habari na wafanyakazi wa Airtel ambapo  vitabu vyenye
thamani ya shilingi milioni mbili vilikabidhiwa kwa shule hiyo.

Akiongea wakati wa halfa ya makabidhiano ya vitabu hivyo,  Afisa
Uhusiano na Matukio  wa Airtel, Dangio Kaniki alisema, " Airtel
inatambua kuwepo kwa  uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia katika
shule zetu na katika kutatua changamoto hizo tunaongeza nguvu na
kushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu kuweza kuinua  sekta
ya elimu.

"Tunafahamu umuhimu wa elimu katika kujikwamua na umaskini, hali ngumu ya maisha na kupata nguvu kazi ya kesho, kwa kutoa kipaumbele kwa
kusaidia na kuhakikisha nyenzo muhimu za kufandishia zinapatikana
mashuleni ili kuweza kufikia dhamira yetu ya kusaidia jamii kwa ujumla
Airtel inatoa fulsa sawa kwa shule zote nchini na leo tumewafikia
wanafunzi wa Kisawasawa Kilombero Morogoro. Tunaamini elimu ndio
ufunguo wa maisha hivyo tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia
kuinua kiwango cha elimu.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Kisawasawa  bw,
Menasi Msigwa ameishukuru Airtel kwa  kuwawezesha  kupata vitendea
kazi  na kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto
nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia
katika mambo mengine.

 Aidha alichukua fulsa hiyo kuwaasa wanafunzi kutumia na kuvitunza
vitabu hivyo ili viweze kusomwa na wanafunzi wengi zaidi na kuongeza
kiwango cha kufaulu katika shule hiyo. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa msaada wa Vitabu kwa shule ya Mtipwa iliyopo mkoa wa Singida.

Tangu Airtel ilipoanza mpango wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali
za sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita,
imeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 1,000
nchini Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia
katika huduma kwa jamii.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU