Monday, September 17, 2012

AIRTEL NA WIKI YA NENDA KWA USALAMA KITAIFA MKOANI IRINGA

 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.
 Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Meneja wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda.Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
 Baadhi ya walemavu wakiingia uwanjani katika uwanja wa Samora mjini Iringa katika Uzinduzi wa Wiki ya kitaifa ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa jana mjini hapa huku Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel ikiwa mdhamini mkuu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kutoka kwa   Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.
 Kiongozi wa Kundi la Wazee Sugu, King Kikii, akiongeza waimbaji wa kundi hilo kutoa burudani ya muziki katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa iliyoanza jana mkoani Iringa.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU