Wasanii kikundi cha Chemchem Arts wakiigiza mchezo mfupi kuonyesha
nguvu ya sanaa za maonyesho katika kufikisha ujumbe, kwenye Jukwaa la
sanaa Jumatatu iliyopita.
.Wasanii wa kikundi cha Chemchem Arts maarufu kama Kidedea, wakiwa
jukwaani wakati wakionyesha mchezo wao uliokuwa na lelo la kuonyesha
jinsi sanaa za jukwaani zinavyoweza kufikisha ujumbe.
KIKUDI cha Chemchem Arts Group, maarufu kwa jina la Kidedea
kimelezea umuhimu kwa wasanii hapa nchini kuandaa michezo ya kuigiza
itakayokuwa na ujumbe mahsusi utakaoisadia jamii ya Tanzania kutafakari juu ya
muskabali wa masuala mbalimbali
yanayoendelea hapa nchini.
Akitoa wasilisho katika Jukwaa la Sanaa Katibu wa Kikundi
hicho Christian Kauzeni amesema moja kati ya mapungufu makubwa ya sanaa za hapa
Tanzania ni kushindwa kufikisha ujumbe utakaoifanya jamii kupata hisia, kuamka
na kuchukua hatua juu ya masuala mbalimbali yanayowakabili wanajamii.
Marta baada ya wasilisho lake lililoeleza changamoto na
mafanikio ya kikundi hicho katika ufanyaji wa sanaa, kikundi hicho kilionyesha
mchezo mfupi wa kuigiza uliojadili
pamoja na mambo mengine tabaka lililopo kati ya tajiri na masikini.
Mchezo huo ulionyesha jinsi wananchi walivyo na hasira ya
kuhukumu na kuwauwa vibaka na wezi wa
kuku huku wakiwaacha mafisadi wanaolihumu taifa wakiendela kutamba na magari ya
kifahari. Mchezo ulilenga katika kuwapa tafakari watazamaji juu ya namna ya
kuchukua hatua katika kukabiliana na masuala mbalimbali yanayojitokeza katika
maisha ya kila siku hapa nchini.
Wakichangia mara baada ya wasilisho na mchezo huo, baadhi ya
wadau wa masuala ya sanaa wameeleza umuhimu wa jamii kuamka na kuchukua hatua
stahili juu ya masuala muhimu badala ya kuacha mambo makubwa kupita na kuisha kirahisi
na badala yake wahoji kwa kina kwa viongozi waliowachagua.
Akijibu hoja za washiriki, Kauzeni alisema ni muhimu sana
kwa watu kushiriki michakato mbalimbali ya maamuziki ikiwa ni pamoja na
kuhudhuria vikao vya serikali za mitaa kwani huko ndiyo wananchi wanaweza
kuanza kuleta mapunduzi ya kweli kwa kufanya maamuzi yenye tija kwa Taifa.
0 maoni:
Post a Comment