Michuano
 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea 
kesho (Septemba 26 mwaka huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa katika miji
 ya Tanga na Morogoro.
Uwanja
 wa Jamhuri mjini Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Polisi 
Morogoro na Toto Africans ya Mwanza. Polisi Morogoro ambayo imepanda 
daraja msimu huu imeshacheza mechi tatu na kufanikiwa kupata pointi moja
 tu baada ya kutoka suluhu na Mtibwa Sugar katika mechi ya kwanza.
Nayo
 Toto Africans ambayo katika mechi iliyopita ugenini ililazimisha suluhu
 dhidi ya Coastal Union, yenyewe ina pointi tatu baada ya kutoka sare 
katika mechi zote tatu ilizocheza chini ya kocha John Tegete.
Mechi
 nyingine ya ligi hiyo itakuwa kati ya Coastal Union ambayo 
itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. 
Kagera Sugar inayofundishwa na Abdallah Kibaden, wikiendi iliyopita 
iliondoka na pointi zote tatu kwenye uwanja huo baada ya kuifunga Mgambo
 Shooting bao 1-0.
Ligi
 hiyo itaingia kwenye Super Weekend kuanzia Ijumaa (Septemba 28 mwaka 
huu) kwa mechi kati ya Azam na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Taifa 
itaoneshwa moja kwa moja (live) na kituo cha SuperSport kuanzia saa 1 
kamili usiku.




 
 
 
 
 
 
 


0 maoni:
Post a Comment