KUMEKUCHA! Kama ni mtoto
hatumwi dukani, kutokana na mashindano mawili makubwa yanayohusisha Redd’s Miss
Tanzania ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho.
Kinyang’nyiro cha kwanza kipo
leo wakati warembo 12 watapopanda jukwaani katika Ukumbi wa PTA uliopo Viwanja
vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), kuwania taji hilo.
Wakati Temeke wakifanyiana
kweli leo, kazi ipo kwa Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, wakati warembo 20
watyakapochuana katika Uwanja wa Soka Kahama, Shinyanga kuwania taji la kanda
hiyo.
Katika Redd’s Miss Temeke,
juzi ilitembelewa na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliyefuatana
na wasaidizi wake kadhaa ili kuwapa somo la mwisho.
Katika shindano la Redd’s
Miss Temeke, kiingilio kwa viti maalumu itakuwa Sh 50,000 na viwango vingine,
huku kukiwa na burudani kadhaa za aina yake.
Akizungumzia shindano la
Redd’s Miss Kanda ya Ziwa, mratibu wa mpambano huo, Clara Mwasa, alisema warembo
hao watawania taji linaloshikiliwa na Trecy Magulla ambaye pia ni Miss Tanzania
namba pili.
Katika shindano hilo
kiingilio kitakuwa ni Sh 30,000 kwa viti maalumu na Sh 20,000 na Sh 10,000 kwa
vile vya kawaida.
“Kuna kitu cha ajabu
kitatokea Kahama, wasanii kibao kutoka Uganda watakuwepo, litakuwa shindano la
kufunga kazi,” alisema Clara.
Redd’s Original
inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ndio ambao wamedhamini
kinyang’anyiro cha Miss Tanzania kwa muda wa miaka mitatu.
0 maoni:
Post a Comment