Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amelishauri Bunge la Afrika Mashariki (EAC) kuzingatia na
kufuata maelekezo yaliyomo kwenye Mkataba ulioanzisha Jumuiya hiyo wakati wa
kuwasilisha na kujadili hoja zao.
Rais
Kikwete ametoa ushauri huo jana jioni (19 Septemba, 2012) alipokutana na Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Margareth Ziwa, Ikulu.
“Jumuiya
ya Afrika Mashariki inahusika na masulala yaliyomo kwenye Mkataba (Treaty) na
Itifaki zilizoanzisha Jumuiya hii na kila nchi inawajibu wa kuzingatia
kilichomo kwenye Mkataba” ameeleza na kufafanua “Lakini
pia msisahau kuwa hizi ni nchi huru zenye sheria na taratibu zake ambazo nchi
zinapaswa kuzifuata na kuzizingatia, hivyo Bunge la Afrika Mashariki linaweza
tu kuzishauri lakini sio kuzielekeza au kuzilazimisha kutekeleza jambo ambalo
halimo kwenye Mkataba ambao nchi hizi zimetiliana saini” ameongeza.
Mheshimiwa
Ziwa amefika Ikulu kujitambulisha kwa Mheshimiwa Rais baada ya kushika wadhifa
huo hivi karibuni.
Mheshimiwa
Ziwa ni raia wa Uganda na ni
Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
ambayo inajumuisha nchi za Burundi,
Kenya, Rwanda, Uganda
na Tanzania.
Rais
amewataka wabunge wapya kusoma Mkataba na Itifaki zilizoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ili
waweze kutekeleza majukumu yao
vizuri bila kuingilia uhuru na taratibu za nchi wanachama.
“Jipeni
muda wa kutosha wa kusoma na kuzielewa taratibu za Mkataba na Itifaki
iliyoanzisha Jumuiya hii, hii itawasaidia sana
katika kujenga hoja zenu na jinsi ya kuziwasilisha”
amewakumbusha kuwa hiyo ndiyo njia pekee ambayo itawafanya kutekeleza kazi na
wajibu wao kwa umakini na uangalifu bila kuingilia taratibu za mabunge ya nchi
wanachama.
Wakati
huo huo, leo asubuhi (20 Septemba, 2012)
Rais amekutana na Katibu Mkuu wa EAC
Dkt. Richard Sezibera ambaye amefika kumueleza Rais juu ya maendeleo na
ratiba ya shughuli muhimu za Jumuiya
hiyo ambazo EAC inatarajia kuzifanya kabla ya mwisho wa Mwaka.
Rais
amempongeza Dkt. Sezibera kwa maendeleo ya Jumuiya hiyo na jinsi shughuli za
utekelezaji zinavyokwenda kulingana na ratiba ya EAC.

0 maoni:
Post a Comment