Thursday, September 20, 2012

MECHI YA JKT RUVU, SIMBA YAINGIZA MIL 73/-

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Simba iliyochezwa jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 73,611,000.
 
Washabiki 12,884 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 16,154,161.02 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 11,228,796.61.
 
Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 150,000, waamuzi sh. 70,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, tiketi sh. 3,175,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 5,384,720.34, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,230,832.20, uwanja sh. 5,384,720.34, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,076,944.07, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 1,076,944.07.
 
61 WASHUHUDIA MECHI YA AFRICAN LYON v POLISI MORO
Watazamaji 61 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na Polisi Moro iliyofanyika jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
 
Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 5,000 ni sh. 185,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 20,287.91, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 27,457.62 na tiketi sh. 89,916.
 
Kamati ya Ligi sh. 6,762.63, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,057.58, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,703.05, gharama za mchezo sh. 6,762.63 na uwanja sh. 6,762.63.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU