Afisa Uhusiano wa
kampuni ya Airtel Tanzania Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi moja kati
ya T-sheti mia nne Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus
International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za
mwaka huu Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu udhamini
wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
tarehe 28 Oktoba. Airtel walikabidhi T-sheti mia nne pamoja na milioni
tano kusaidia mbio hizo.
Afisa Uhusiano wa
kampuni ya Airtel Tanzania Bi Jane Matinde (kulia) akimkabidhi hundi ya
shilingi milioni tano Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus
International ambaye pia ni Mratibu wa mbio za Rock City Marathon za
mwaka huu Bi Grace Sanga jijini Dar es Salaam jana kama sehemu udhamini
wa mbio hizo zitakazofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
tarehe 28 Oktoba. Airtel pia walikabidhi fulana mia nne zitakazotumika
katika mbio hizo.
KAMPUNI
ya mawasiliano nchini ya Airtel imeahidi kuendelea kusaidia michezo
mbalimbali nchini ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya vijana.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana katika hafla fupi ya kukabidhi shilingi
milioni tano pamoja na fulana mia moja kama udhamini wa mbio za Rock
City Marathon za mwaka huu zenge kauli mbiu ‘tukuze utalii wa ndani
kupitia michezo’, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema kuwa
kampuni yake itaendelea kusaidia michezo mbalimbali nchini ikiwemo
riadha ili kukuza maendeleo ya vijana.
“Udhamini
wetu wa shilingi milioni tano pamoja fulana mia moja katika mbio za
Rock City mwaka huu unalenga katika kusukuma maendeleo ya vijana kupitia
michezo kwa tunaamini kuwa michezo imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajira
duniani.
“Tunaahidi
kuendelea kusaidia michezo mingine kwa kuwa pia tunaamini kupitia
michezo mbalimbali tunaweza kutangaza vivutio vyetu vya utalii duniani.
Mfano nzuri ni mbio za mwaka huu za Rock City Marathon
zitakazowakutanisha wanariadha mbalimbali kutoka nchi jirani,” aliongeza
Bi. Matinde.
Akipokea
hundi na fulana hizo, Mratibu wa mbio hizo kutoka katika kampuni ya
Capital Plus International (CPI), Bi. Grace Sanga aliishukuru kampuni ya
Airtel kwa kuendelea kusaidia mbio za Rock City na kuyahasa mashirikia
na makampuni mengine kuiga mfano wa kampuni hiyo.
“Tunaishukuru
Airtel kwa msaada wao kwa kuwa msaada huu utatusaidia tujiandae vizuri
na Rock City Marathon ya mwaka huu itakayofanyika Oktoba tarehe 28
katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,” alisema Grace.
Grace
alisema kuwa mbali na Airtel wadhamini wengine ni pamoja na Shirika la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Parastal Pension Fund (PPF), Geita Gold Mine,
African Barrick Gold, Air Tanzania Company Ltd (ATCL), Mamlaka ya Taifa
ya Mbuga za Wanyama nchini (TANAPA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),
Nyanza Bottles, New Africa Hotel na New Mwanza Hotel.
Aidha,
Bi Sanga aliwaasa wanariadha kujitokeza na kuanza kujisajili ili
kushiriki katika mbio hizo na kusema kuwa fomu za usajili zinapatikana
katika ofisi za uwanja wa CCM Kirumba, ofisi za kampuni ya Capital Plus
International zilizopo katika jengo la ATCL ghorofa ya tatu, ofisi za
Bodi ya Utalii jengo la IPS ghorofa ya tatu, Dar es Salaam, na
zinapatikana katika tovuti ya www.rockcitymarathon.blogspot.com.
CPI
ilitangaza kuwa atakaeibuka kinara katika mbio za kilometa 21 mwaka huu
kwa wanaume na wanawake atazawadiwa shilingi milioni moja na laki mbili
wakati mshindi wa pili ataweka mfuko shilingi laki tisa na mshindi wa
tatu ataondoka na shilingi laki saba.
0 maoni:
Post a Comment