KIDUNDA BAADA YA PAMBANO LAKE LA OLYMPIC UINGEREZA.
Kitendo cha BFT kutokuwa na medali katika mashindano ya taifa ya ngumi ni kuonesha wazi ukata uliokuwepo katika michezo ngumi za radhaa hapa nchini.
Hii
inaonesha wazi jinsi gani ngumi zinahitaji msaada wa kuyaendesha
mashindano mbalimbali yanayofanyika nchini ambayo ndiyo yanayotoa
wawakilishi katika mashindano ya kimataifa.
Tunajua
fika kama ngumi na riadhaa ndio michezo inayojitahidi kufikia viwango
vya mashindano makubwa ya kimataifa kwa wanamichezo wenyewe kujituma
hivyohivyo katika mazingira yao magumu na umaskini
walionao-(tukumbuke wengi wanaocheza michezo hii wanatoka katika familia
za chini kimaisha,sio cha kustaajabu mabondia wetu kula kwa
mamantilie).
Na
umaskini huuhuuu ndio wanaokwenda nje kupeperusha bendera,na
wanapocheza tunafurahi kuwaangalia na kuwashabikia lakini hatutaki kujua
maandalizi yao yapoje mpaka matokeo yawe kinyume na matarajio.
TUNAWAOMBA
WADHAMINI NA WAFADHILI MJITOKEZE PIA KATIKA NGUMI hii itasaidia
kuongeza hamasa zaidi kimichezo,tutakuwa na uhakika wa medali
commonwealth na Olympic ,tutaongeza mikanda mingine mingi ya ubingwa wa
dunia na kipato kitaongezeka kwa kodi za mabingwa na pia
nchi itatangazika vema katika Utalii, hivyo kama kuna tatizo lililobaki
katika ngumi kwa wafadhili ni vizuri kuwekwa wazi likatatuliwa
tukawaacha vijana wanafanya kazi.
Kwa
mapungufu yaliyojitokeza katika mashindano ya taifa ya ngumi za
ridhaa,BFT imeyaona kupitia katibu mkuu wake Makore Mashaga ambae
alikuwa akihangaika huku na kule kuhakikisha mashindano yanafanikiwa
katika mazingira yoyote,mapungufu watayafanyia kazi na pia wengine
wanaostahili kupongezwa ni rais wa ngumi za kulipwa TPBO bw Yasin
abdalah'ustadh kwa kutoa zawadi na hamasa kwa wachezaji na viongozi wa
klabu shiriki akishirikiana na Onesmo ngowi. .
Viongozi
hawa wa ngumi za kulipwa walikuwa karibu kuwasaidia wenzao wa ngumi za
ridhaa kuyaendesha vema mashindano hayo ambayo ndio msingi mzuri wa
ngumi za kulipwa na kweli vipaji vimeonekana mabondia walionesha
ushindani wa hali ya juu,hivyo wadau wapenda maendeleo ya michezo na
serikali yenyewe ni vema kuisaidia hii michezo
0 maoni:
Post a Comment