Thursday, October 25, 2012

AFRIKA KUSINI KUFUNGUA DIMBA NA CAPE VERDE

Timu ya AFRIKA KUSINI wenyeji wa mashindano ya mataifa ya AFRIKA watafungua dimba la mashindano hayo na timu ya CAPE VERDE baada ya droo ya kupanga makundi kufanyika hiyo jana nchini AFRIKA KUSINI.

Katika kupanga makundi hayo Rais wa AFRIKA KUSINI naye alikuwa mmoja wapo wakati wa droo ambapo timu yake ya BAFANABAFA ipo kundi A ikiwa na timu ya ANGOLA, MOROCCO na CAPE VERDE 

Timu ya GHANA ambayo mara ya mwisho kutwaa kikombe cha mataifa ya AFRIKA ilikuwa mwaka 1982 imepangwa na timu za DR CONGO, NIGER na MALI .
Mabingwa wa kombe hilo ZAMBIA wao wako kundi C na NIGERIA ETHIOPIA AND BURKINA FASO.

IVORY COAST waliotinga fainali na ZAMBIA wao wako kundi D na timu ya TOGO, TUNISIA, na ALGERIA.
Tangu mwaka 2000 CAMEROON wamtwaa mara mbili mwaka 2000 na 2002 wakati 2004 kombe litwaliwa na TUNISIA huku nchi ya MISRI ikilitwaa mara tatu kabla ya mwaka 2012 nchi ya ZAMBIA kulitwaa kombe hilo.
 

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU