Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa Benki ya Barclays Tanzania, Samwel Mkuyu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo wakati benki hiyo ikitangaza kuongeza muda wa kampeni
yake ya Amana za Muda Maalumu. Pamoja naye ni Mkuu wa Mawasiliano wa
Barclays, Tunu Kavishe.
Barclays, Tunu Kavishe.
Benki ya Barclays
Tanzania imetangaza kuongeza muda wa kampeni yake ya Amana za Muda Maalumu hadi
Desemba 31 Mwaka huu. Kampeni hii ilizinduliwa rasmi Agosti 6, 2012 na ilikuwa
ifikie mwisho wake Desemba 6 Mwaka huu. Wateja wa Barclays wa Kitengo cha
Kibenki cha akaunti binafsi kama vile Wateja
Binafsi, Wateja Wakubwa na Wafanyabiashara wanaweza kufurahia faida ya kuweka Amana
za Muda Maalumu na Barclays.
Kampeni
hii imetengenezwa kupitia bidhaa ya kipekee ya Barclays inayofahamika kama ‘Regular Interest Fixed Deposit’. Mteja anayefungua
Akaunti ya Amana ya Muda Maalumu yenye Faida ya Kawaida ataweza kulipwa faida ya
amana yake kila mwezi kwa kipindi chote cha muda wa amana yake tofauti na
ilivyo kwamba faida hutolewa tu mwishoni mwa kipindi cha akaunti hiyo maalumu..
“Kiwango
cha chini ambacho wateja wanatakiwa kuwa nacho ni shs milioni 15 na muda wa
chini ambao amana hiyo itatakiwa kuwemo katika akaunti ya Barclays ni mwaka
mmoja na muda wa juu ni miaka 5,” alisema Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa
Barclays, Samwel Mkuyu.
Bwana
Mkuyu aliongeza kwa kusema: “Faida ya kila mwezi kwa wateja italipwa kwenye
akaunti zao za kawaida na faida kwenye fedha ya msingi iliyowekwa kwenye
akaunti ya Muda Maalumu itatolewa mwishoni mwa kipindi husika. Tuna aina tofauti kwa viwango tofauti na
maelezo yake kwa kina yanapatikana kwenye matawi yetu yote nchini Tanzania.
”
Aliendelea:
“Sisi Barclays, tumedhamiria kuifanya sekta ya benki Tanzania kuwa rahisi zaidi kwa
wateja wetu kwa kuleta huduma rahisi zinazopatikana kwa wote. Wateja wetu
wataendelea kufurahia huduma za bure za kidijitali ikiwa ni pamoja na kutoa
fedha bure kwenye mashine za ATM, huduma ya bure ya ujumbe mfupi kupitia simu
za mkononi, kupata taarifa za akaunti bure kupitia mtandao na huduma za kibenki
kupitia mtandao wa intaneti”.
0 maoni:
Post a Comment