Mashindano ya Redds Miss
Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua ya mwisho ilikuwa
hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na kufanikiwa kuwapa warembo jumla
ya 30 .
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO AGENCY Hashim Lundenga alisema
mashindano kiujumla katika ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa
na kuonyesha kuwa fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya
Juu.
Washiriki wengi wa mwaka huu
kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wengine
wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo ambalo litaleta hamasa kubwa katika
shindano la mwaka huu.
Baada ya kukamilika kwa
mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi kuwa warembo wote 30
walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha Redds Miss Tanzania 2012
wataingia kambini siku ya jumanne October 2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya
kitalii ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo hapa
Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
Tunapenda kuwajulisha wadau
wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS TANZANIA 2012 litafanyika
siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal
(Ubungo Plaza).
Kwa Upande wake Meneja wa
Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro alisema wao kama wadhamini wakuu wa
Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa
wadau wote wa tasnia ya urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote
waliofanikiwa kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo
mbalimbali.
0 maoni:
Post a Comment