Tuesday, October 16, 2012

LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 24


Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Tanzania Bara inaanza rasmi Oktoba 24 mwaka huu kwa timu 18 kati ya 24 kujitupa kwenye viwanja tisa tofauti katika ligi hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Mechi za raundi ya kwanza za kundi A zitakazochezwa Oktoba 24 mwaka huu ni Burkina Faso dhidi ya Mbeya City (Jamhuri, Morogoro), Mlale JKT na Small Kids (Majimaji, Songea) na Kurugenzi Mufindi dhidi ya Majimaji (Uwanja wa Wambi, Mufindi mkoani Iringa).
Mkamba Rangers na Polisi Iringa zitakamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mechi za raundi ya pili kwa kundi hilo zitachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwa Polisi Iringa vs Mbeya City (Samora, Iringa), Majimaji vs Small Kids (Majimaji, Songea), Burkina Faso vs Mkamba Rangers (Jamhuri, Morogoro) na Kurugenzi Mufindi vs Mlale JKT (Wambi, Mufindi).
Raundi ya tatu ni Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Mbeya City vs Mlale JKT (Sokoine, Mbeya), Small Kids vs Mkamba Rangers (Nelson Mandela, Sumbawanga), Majimaji vs Burkina Faso (Majimaji, Songea) na Polisi Iringa vs Kurugenzi Mufindi (Samora, Iringa).
Kundi B Oktoba 24 mwaka huu ni Ndanda vs Transit Camp (Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Moro United (Mabatini, Pwani) wakati Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors vs Tessema (Mabatini, Pwani) na Polisi Dar es Salaam vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).
Raundi ya pili kwa kundi hilo ni Oktoba 27 mwaka huu Ndanda vs Green Warriors (Nangwanda Sijaona, Mtwara), Villa Squad vs Tessema (Mabatini, Pwani) wakati Oktoba 28 mwaka huu ni Ashanti United vs Transit Camp (Mabatini, Pwani) na Oktoba 29 mwaka huu ni Moro United vs Polisi Dar es Salaam (Chamazi, Dar es Salaam).
Novemba 1 mwaka huu ni Green Warriors vs Ashanti United (Mabatini, Pwani), Novemba 2 mwaka huu ni Polisi Dar es Salaam vs Villa Squad (Chamazi, Dar es Salaam), Novemba 4 mwaka huu ni Tessema vs Ndanda (Chamazi, Dar es Salaam) na Transit Camp vs Moro United (Mabatini, Pwani).
Kundi C ni Oktoba 24 mwaka huu Kanembwa FC vs Polisi Dodoma (Lake Tanganyika, Kigoma), Mwadui vs Morani (Kambarage, Shinyanga), Pamba vs Polisi Mara (Kirumba, Mwanza) na Rhino Rangers vs Polisi Tabora (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
Raundi ya pili ni Oktoba 27 mwaka huu; Polisi Tabora vs Polisi Dodoma (Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mwadui vs Polisi Mara (Kambarage, Shinyanga), Kanembwa FC vs Morani (Lake Tanganyika, Kigoma) na Pamba vs Rhino Rangers (Kirumba, Mwanza).
Oktoba 31 mwaka huu ni raundi ya tatu; Polisi Mara vs Rhino Rangers (Karume, Musoma), Morani vs Polisi Tabora (Kiteto, Manyara), Polisi Dodoma vs Pamba (Jamhuri, Dodoma) na Kanembwa FC vs Mwadui (Lake Tanganyika, Kigoma).
 
MBAGA AZICHEZESHA KENYA, BAFANA BAFANA
Mwamuzi Oden Mbaga wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ndiye anayechezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana).
Mechi hiyo inachezwa leo Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi. Mbaga anasaidiwa na waamuzi wasaidizi wa FIFA, John Kanyenye kutoka Mbeya na Erasmo Jesse wa Morogoro.
TFF imeteua waamuzi hao baada ya kupata maombi kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ambao ndiyo waandaaji wa mechi hiyo ambayo ni moja ya vipimo kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Henry Michel kutoka Ufaransa.
TAFCA YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA FOMU
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) imeongeza muda kwa wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi wa chama hicho ambao sasa utafanyika Novemba 25 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua fomu lakini mwitikio wa wagombea bado umekuwa mdogo ambapo ni watano tu waliojitokeza.
Hivyo, amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu ambapo mwisho itakuwa ni Oktoba 19 mwaka huu saa 10 kamili alasiri. Fomu zinapatikana ofisi za TAFCA ambazo ziko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mhazini na wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU