Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Edith Bebwa akiwa na Meneja Masoko
wa Tbl Fimbo Buttala kwenye mkutano na waandishi wa habari juu ya
uzinduzi wa mashindano ya mbio za mitumbwi ya Balimi ya kanda ya Ziwa
ambapo yanatarajiwa kuanza mkoani Kigoma hivi karibuni.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi
Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa kanda ya ziwa mwaka
2012.
Mashindano hayo ya kupiga kasia, yanayo
dhaminiwa na bia ya “Balimi Extra Lager”
yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara na visiwa vya
Ukerewe. Mashindano haya yamekuwa yakijizolea umaarufu katika kanda ya ziwa
mwaka hadi mwaka na yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa
na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka kila
mwaka.
Akiongelea mashindano ya mwaka huu wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa
Bia ya Balimi Extra Lager Edith Bebwa alisema, Ni zaidi ya miaka saba sasa, bia
ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani
Kigoma, kwa kipindi chote hiki Balimi imefanikiwa kuleta changamoto kubwa katika
mchezo wa kupiga makasia, kwa kuwapa
fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato
cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa
wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika.
Kwa hivi sasa timu zote zimeshaanza maandalizi, tayari kwa
mashindano ya ngazi ya mkoa ambapo kwa mwaka huu yataanzia Kigoma tarehe 20
Octoba, ikifuatiwa na Kagera tarehe 27 Octoba, Mwanza tarehe 4 Novemba, Kisiwa
cha Ukerewe tarehe 10 Novemba na Mara tarehe 17 Novemba. Baada ya fainali hizo
za ngazi ya mikoa timu zilizoshinda zitakutana katika fainali kuu
itakayofanyika Jijini Mwanza tarehe 2 Desemba pale Mwaloni Kirumba.
Akizungumzia timu zitakazofuzu kuingia fainali kuu, Bi Edith
alisema; timu tatu za wanaume na mbili za wanawake zitakazoshika nafasi za juu zaidi
katika ngazi ya mkoa ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika
Jijini Mwanza.
Na timu zilizochukuwa ubingwa mwaka jana upande wa wanaume na
wanawake watapata fursa ya moja kwa moja
ya kuingia finali kuu za mwaka huu ili kutetea ubingwa wao.
Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za Mkoa na
fainali kuu, Meneja Masoko Bw. Fimbo Butallah alisema; Kama ilivyo ada, zawadi
zimekuwa zikiongezeka kila mwaka, ukiwemo mwaka huu 2012, ambapo zawadi
zimepangwa kama ifuatavyo;
Ngazi ya Mikoa
|
|
Fainali Kuu
| |||||||||
Wanaume
|
Wanawake
|
|
Wanaume
|
Wanawake
| |||||||
Mshindi
wa kwanza
|
900,000
|
700,000
|
|
2,700,000
|
2,300,000
| ||||||
Mshindi
wa Pili
|
700,000
|
600,000
|
|
2,300,000
|
1,700,000
| ||||||
Mshindi
wa Tatu
|
500,000
|
400,000
|
|
1,700,000
|
900,000
| ||||||
Mashindi
wa Nne
|
400,000
|
300,000
|
|
900,000
|
700,000
| ||||||
5
hadi 10 - Kila timu
|
250,000
|
200,000
|
|
500,000
|
250,000
| ||||||
Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani
kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki. Tunawaomba
wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia
mashindano haya yenye mvuto na msisimko wa aina yake.
0 maoni:
Post a Comment