Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys)
imefuzu kucheza raundi ya tatu nay a mwisho kwenye michuano ya kutafuta
tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Vijana baada ya Misri kujitoa.
Serengeti
Boys ilikuwa icheze raundi ya pili dhidi ya Misri; mchezo wa kwanza
ukichezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam na ule wa marudiano
wiki mbili baadaye jijini Cairo.
Katika
raundi ya kwanza Serengeti Boys inayofundishwa na Jakob Michelsen
kutoka Denmark ilikuwa icheze na Kenya mwezi uliopita, lakini nchi hiyo
ilijitoa katika michuano hiyo ambayo fainali zake zitachezwa Machi
mwakani nchini Morocco.
Serengeti
Boys sasa itacheza raundi ya tatu kwa kumkabili mshindi wa mechi kati
ya Zimbabwe na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itachezwa Novemba 18
mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika ugenini
wiki mbili baadaye.
Zimbabwe
na Congo Brazzaville zitapambana zitapambana kati ya Oktoba 12-14 mwaka
huu, Zimbabwe ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza wakati ya marudiano
itafanyika kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment