Sadiki momba na alen kamote kuzipiga mwisho wa mwezi
Bondia
mwenye manjonjo,mbwembwe na vituko vingi ulingoni Sadiki
Momba"kijotijoti". Amesema anamtaka Ramadhan Shauri(ambae ni bingwa
waIBF Afrika)'.sio alen kamote wa tanga ambae ni bingwa wa Afrika
mashariki anaetegemea kucheza nae tarehe 27 octoba 2012,pambano hilo
linaloandaliwa na ally mwanzoa na kuratibiwa na bigright promotion
katika ukumbi wa Friends corner hotel-manzese.
Sadiki momba anasema bondia anayemfikiria ni Ramadhan Shauri na
ni bingwa wa kupewa kwa kutengenezewa mazingira ,"shauri haniwezi na
yeye mwenyewe anajua hata mapromota wakitokea wa kutukutanisha mie
nakuwa tayari kwa gharama zozote lakini Mzazi kocha wa shauri hukataa au
utaja dau kubwa la mamilioni ili promota akimbie,Shauri amecheza
mapambano 13,kapigwa matatu,kadroo moja tisa kashnda wakati mie
nimecheza mapambano kumi na nane(18) droo moja,nimepigwa moja na mudy
matumla kwa kubebwa na yaliyobaki 16 yote nimeshinda hivyo mie nina
rekodi nzuri ulingoni kuliko Shauri.sijapata tu nafasi ya hizo mechi za
ubingwa lakini hao mabingwa wao wanaowapa mechi za kimataifa mie
nimeshawapiga sana mpaka kuokolewa na refa au kufikishwa mahospitalini
wakiwa hali mbaya kwa kipigo.njooni mumuangalie kamote nitakavyomfanya
ndio maana simzungumzii sana najua nitampiga kirahisi sana akakate viuno
vyake kwao tanga.
.Naomba promota yoyote ajitokeze kutuandalia mchezo kati yangu na shauri wasimtengenezee mazingira na vibonde,
Tunajua
kocha Mzazi na mabondia wake wanaabudu uchawi hivyo nitawaomba chama
kitakachosimamia mchezo kiwaruhusu waganga wao waroge mpaka ulingoni
siku ya mchezo- nasema hivyo ili mzazi asiogope sana akubali kucheza na
mimi kwa imani zake za kichawi.mimi nijiamini kwa mazoezi yangu na
kipaji nilichonacho na nina uwezo wa kulifanyia taifa letu makubwa kama
nitawezeshwa kwa kuandaliwa mapambano ya kimataifa na ya nje ya nchi,
kwani hapa Tanzania karibu mabondia wote wa uzito wangu
nimeshawamaliza,bado sijulikani kwa wakubwa kwa sababu sijapata mechi za
kimataifa.
0 maoni:
Post a Comment